Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Kilimanjaro SAR, Ivan Brown akitoa taarifa za shirika hilo kwa wanahabari (hawapo pichani) kuhusu shughuli mbalimbali za uokoaji ilizofanya katika kipindi cha mwaka mmoja.

Mkurugenzi wa Rasilimali watu katika shirika la Kilimanjaro SAR, Amour Abdalah akizungumza na wanahabari (hawapo pichani kuhusu mwaka mmoja wa operesheni ya shirika hilo. 
Kikosi cha uokoaji kwa kutumia Helkopita kikiwa katika Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kutoa msaada kwa wageni. 
Ndege aina ya Helkopta inayotumiwa na Shirika la Kilimanjaro SAR katika kufanya shughuli za uokoaji katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro. 


Na Dixon Busagaga wa globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

SHIRIKA la Kilimanjaro SAR linayojishughulisha na utoaji wa huduma ya utafutaji na uokoaji wa watalii wanaopata matatizo ya kiafya katika maeneo yenye muinuko ikiwemo Mlima Kilimanjaro limetangaza kutoa bure huduma zake kwa waongoza watalii pamoja na wapagazi .

Hatua hiyo imefikiwa baada ya baadhi ya watu wanaojishughulisha na shughuli za kusaidia wageni katika Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro kupata matatizo ya kiafya na kushindwa kupata huduma huku kundi kubwa la watu hao kukosa Bima za Afya ,wengine wakikosa kabisa kipato cha uhakika.

Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika la Kilimajaro SAR,Ivan Brown alitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya shughuli zilizofanywa na kampuni hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kuanza operesheni za uokoaji kwa kutumia njia ya Helkopta.

“Sisi ni wa kwanza na pekee katika Dunia hii tunaotoa huduma ya uokoaji Bure kwa wote wanaofanya shughuli za mlima ,tunafahamu Wapagazi,Waongoza watalii hawana bima, hawana njia zozote za kujipatia kipato ambazo zingesaidia katika uokoaji”alisema Brown .

“Watakaopata matatizo ya kiafya au ajali wawapo mlimani wanaweza kuwasiliana nasi ,tutaaenda juu na kumuokoa bila ya gharama zozote kwa sababu mipango yetu ni kuokoa maisha ,ndio sababu tunasema kwa waongoza watalii au wapagazi , uhai ndio kipaumbele cha kwanza”aliongeza Brown .

Alisema shirika hilo likiwa linaadhimisha mwaka mmoja wa utoaji huduma katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro tayari imetoa matibabu kwa zaidi ya watu 250 huku akieleza kuweka rekodi ya kwanza Afrika kwa kumuokoa mgonjwa aliyekuwa katika hali mbaya, umbali wa Mita 5000.

“ Tayari tumetoa huduma kwa zaidi ya wagonjwa 250 na miongoni mwao aliingia kwenye historia Afrika ya kuwa mtu wa kwanza kuokolewa kwa na Helkopta katika eneo lenye urefu wa Mita 4800, katika kambi ya Cosovo Mlima Kilimanjaro June 22 mwaka jana”alisema Borown .

“Tumeokoa waongoza watalii na wapgazi 50 bila malipo ,bado tunashukuru kwa ushirikiano na msaada kutoka kwa taasisi mbalimbali kwa kuruhusu mazingira kwa shirika letu kuweza kufanya shughulizaek za uokoaji maisha kwa urahisi.

Mbali na shughuli ya utafutaji na uokoaji, Kampuni ya Kiliamanjaro SAR imeingia makubaliano na Hospitali ya St Joseph kwa kuanzisha Kliniki ya kisasa “Kilimanjaro SAR High Altitude Medicine Clinic” kwa ajili ya kutoa huduma ya matibabu kwa magonjwa yatokanayo na muinuko .

Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa shirika hilo ,Amour Abdalah alisema kliniki hiyo ya kwanza Afrika imeanzishwa baada ya kubaini kwamba mgonjwa anapookolewa kutoka mlimani anahitaji pia kupata huduma stahiki za matibabu.

“Magonjwa ya mlimani yanahitaji, matibabu maalumu ,na ndio sababu tukaanza na operesheni ya kutoa huduma kwa kutumia Helkopta ikiwa ni huduma ya kwanza kwa afrika na baadae mgonjwa huyu hufikishwa katika kliniki yetu na kupatiwa matibabu” alisema Abdalah.

Alisema wazo la kuanzishwa huduma hizo lilianza mwaka 2013 baada ya kuona kwamba utoaji wa huduma sahihi ya uokoaji na vifaa vya kitabibu vilihitajika na si pekee kwa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro bali pia kwa Sekta ya Utalii Tanzania.

Abdalaha alisema kwa sasa kampuni ya Kilimanjaro SAR imepanua wigo wa utoaji wa huduma za utafutaji na uokoaji katika maeneo mengine zikiwemo hifadhi za taifa za Serengeti,Arusha,Manyara,Ruaha na Mikumi.

“Mlima Kilimanjaro umekuwa na wageni wengi wakifanya shughuli za utalii ,na wengi wao baada ya kuapanda mlima Kilimanjaro wanaendelea na safari nyingine kutizama vivutio vya utalii,jambo kubwa tunalofanya katika sekta ya utalii ,tumewahakikishia usalama wageni wanaokuja Tanzania kupanda Mlima Kilimanjaro “alisema Amour.

Katika kipindi cha mwaka mmoja Shirika la uokoaji ya Kilimanjaro SAR tayari imejinyakulia tuzo tano za uongozi moja ikiwa ni ya Tanzania ambazo ni “C.E.O of the Year 2018 Afrika “ ,“ H.R of the Year 2018 Afrika” ,“Dream Company to work for “ , “Employer Brand Afrika “ ,” Shirika Bora la kati Tanzania “ tuzo iliyotolewa na ATE.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: