Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe za siku wa wanawake duniani ambaye pia ni kuu wa kitengo cha maendeleo ya jinsia Chuo Kikuu cha Mzumbe Dkt Elizabeth Genda akitoa ahadi ya kujenga mabweni ya wasichana wa shule za sekondari zinazo zunguka chuo hicho.
Prof Aurelia Kamuzola akitoa mada ya kuwahamasisha wanawake kujitambua na kuwa na hamasa ya kufikia malengo katika hafla ya kusherekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.
 Baadhi ya wanafunzi wa sekondari zilizo karibu na chuo kikuu cha Mzumbe wakiwa katika maandamano ya kusherehekea siku ya wanawake duniani.
 Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Bi. Enedy Mwanokwate ambaye amemwakilisha mkuu wa wilaya ya Morogoro, akipokea maandamamo ya wanawake wa chuo kikuu cha Mzumbe, pamoja na wanafunzi wa kike wa shule ya Adriani mkona na Mongola sekondari.
Mgeni resmi katika maadhimisho hayo, Bi Enedy Mwanokwate ambaye amemwakilisha mkuu wa wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akiangalia maonyesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wajasiliamali wanafunzi wa kike wa chuo Kikuu cha Mzumbe.
 Mgeni resmi katika maadhimisho hayo Bi Enedy Mwanokwate ambaye amemwakilisha mkuu wa wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akiangalia maonyesho ya bidhaa ya vitenge vya batiki vinazozalishwa na wajasiliamali wanawake wa kata ya bibwa manispaa ya morogoro
Mgeni resmi katika maadhimisho hayo, Bi Enedy Mwanokwate ambaye amemwakilisha mkuu wa wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akiangalia maonyesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wajasiliamali wanafunzi wa kike wa chuo kikuu cha mzumbe.
Mwakilishi wa mgeni rasmi Bi Enedy Mwanokwate akipokea picha cha mkuu wa wilaya ya Morogoro Regina chonjo iliyochorwa na mmoja ya wanafunzi wa kike wa chuo kikuu cha mzumbe katika hafla ya kusherehekea siku ya wanawake duniani iliyofanyika katika chuo hicho.


Umoja wa wanawake wa Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro wamedhamilia kuwakomboa wanafunzi wa kike wanaosoma shule za sekondari zinazozunguka chuo hicho kwa kuwajengea mabweni ili kukuza kiwango cha elimu.

Wanawake hao wametoa ahadi hiyo wakati wakisherehekea siku ya wanawake duniani ambapo wameeleza kuwa sababu ya kuchukua uamuzi huo ni kutokana na changamoto nyingi zinazo wakabili wasichana na ikiwemo vishawishi vinavyosababisha mimba za utotoni jambo linalipelekea wanafunzi wengi kukatisha masomo yao.

Miongozni mwa shule ambazo zinazunguka chuo hicho cha Mzumbe ambacho ndio kinaongoza kwa ubora nchini ni pamoja na shule ya sekondari mongola, Adrian Mkoba, na kipela pamoja na shule ya msingi Mzumbe.

Siku ya wanawake duniani huadhimishwa kila terehe nane ya mwezi wa tatu kila mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Fikiri sawa, jenga uwezo na kuleta maendeleo endelevu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: