Msaada wa Chakula, Dawa, magodoro, shuka, blanketi na vyandarua vimewasili Mjini Beira nchini Msumbiji ambako vitagawiwa kwa waathirika wa kimbunga Idai kilichosababisha mafuriko na vifo vya watu zaidi ya 2,000 katika mji huo. Msaada huo ambao umetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli umepelekwa na ndege za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ((JWTZ).
Ndege ya JWTZ ikiwa na misaada wa Chakula, Dawa, magodoro, shuka, blanketi na vyandarua ikiwasili Mjini Beira nchini Msumbiji. 

Msaada wa Chakula, Dawa, magodoro, shuka, blanketi na vyandarua vimewasili Mjini Beira nchini Msumbiji ambako vitagawiwa kwa waathirika wa kimbunga Idai k 
Msaada wa Chakula, Dawa, magodoro, shuka, blanketi na vyandarua vikishushwa Mjini Beira nchini Msumbiji ambako vitagawiwa kwa waathirika wa kimbunga Idai 
Msaada wa Chakula, Dawa na vifaa vya kujihifadhi vikishushwa mjini Harare nchini Zimbabwe baada ya kupelekwa na ndege za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa maafa.
Makabidhiano ya saada wa Chakula, Dawa na vifaa vya kujihifadhi mjini Harare nchini Zimbabwe baada ya kupelekwa na ndege za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania {JWTZ} kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa maafa
---
Msaada wa Chakula, Dawa na vifaa vya kujihifadhi umewasili Harare nchini Zimbabwe baada ya kupelekwa na ndege za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania {JWTZ} kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa maafa yaliyosababishwa na kimbunga Idai ambacho kimeikumba sehemu ya nchi hiyo.

Pamoja na kusababisha mafuriko, vifo na maelfu ya kaya kukosa makazi, kimbunga hicho kimesababisha kaya nyingi kuhitaji chakula, dawa na mahali pa kujihifadhi kwa haraka.

Nchi nyingine zilizokumbwa na kimbunga hicho ni Msumbiji na Malawi ambako maelfu ya watu wamepoteza maisha na mamilioni kukosa makazi.

Jana Machi 19, 2019 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alitoa msaada wa tani 214 za chakula, Dawa tani 24 na vifaa vya kujihifadhi vikiwemo blanketi, shuka, vyandarua na magodoro ambavyo vilipelekwa katika nchi hizo kwa ndege na Malori ya Jeshi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: