Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza akiongea na wanafunzi na wazazi wa shule ya sekondari ya Nyerere wakati wa maafari ya kidato cha sita akimwakirisha mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas aliyetakiwa kuwa mgeni rasmi
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza akimkabidhi mkuu wa shule ya sekondari ya Nyerere fedha alipewa na mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas kwa ajili ya kuasidia ujenzi wa nyumba ya walimu wa shule hiyo
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi,wazazi mbalimbali pamoja wanafunzi wa kidato cha sita
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
MJUMBE wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas amechangia kiasi cha shilingi milioni mbili kwa ajili ya maendeleo ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyerere iliyopo katika kata ya migoli mkoani Iringa
Akimwakilisaha MNEC Salim Asas wakati wa mahali ya kidato cha sita katika shule hiyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa nyumba za walimu na tayari ameona jitihada zinazoendelea hivyo kiasi cha shilingi milioni mbili alipewa na MNEC basi zitasaidia katika ujenzi huo.
“Nimepewa pesa hizi na mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas nije niwaletee kwa niaba yake hivyo nimezifikisha salama na nyie mzitumieni katika kumalizia ujenzi wa nyumba hizo za walimu ili walimu waishi vizuri” alisema Baraza
Baraza alisema, mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas anayependa kuchangia maendeleo katika sekta mbalimbali ndio maana katika shule hiyo amechangia zaidi ya mara moja kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu katika shule hiyo.
“Mmesema hapa wenyewe kuwa mara kadha amekuwa akiwasaidia kuchangia maendeleo katika shule hii na leo kanituma niwaletee hizi pesa kwa ajili ya mchango wake kwenye shule hii kwa lengo la kuboresha taaluma kwa wanafunzi wa hapa” alisema Baraza
Aidha Baraza aliwataka wanafunzi wa shule hiyo kuhakikisha wasoma sana na kufaulu mitihani iliyopo mbele yao na kurudisha fadhila kwa walimu na wazazi wao waliowalea na kuwafundisha hadi hapo walipofika.
“Hakuna kitu kizuri kwa mwanafunzi kufaulu mtihani na kusonga mbele hiyo maana walimu wanawafundisha mkiwa shuleni lakini mkiwa nyumani wazazi wenu wanatumia gharama kubwa kuwa somesha huku wakitegemea kupata matokeo chanya ya mtihani wenu wa mwisho” alisema Baraza
Baraza aliongeza kwa kuwataka wanafunzi wa kidato cha sita kusimamia kikamilifu malengo waliyojiwekea ili kuifikia ndoto ambayo wamekuwa nayo kwa miaka mingi ya kupata au kufika maisha bora ambayo kila mwanadamu anatamani kuyafikia.
Lakini Baraza aliwapongeza walimu na wanafunzi waliowahi kusoma shule hiyo kwa kupata matokeo mazuri kila mwaka na kusaidia kukuza taaluma kwa wanafunzi wa shule hiyo na kuwaandaa vijana ambao watakuaja kulisaidia taifa hapo baadae.
Awali akisoma taarifa ya shule hiyo mkuu wa shule Laurent Manga alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya umaliziaji wa nyumba ya walimu inayojengwa kwa nguvu za wazazi,wanafunzi na serikali.
“Mgeni rasmi sis hapa tunaupungufu wa bati mia moja na ishirini,saruji mifuko mia tatu,mbao mia moja themenini na tisa pamoja na misumari kilo hamsini,hivyo ndio vinakwamisha umaliaji wa nyumba hiyo ya walimu” alisema Manga
Manga alisema, uongozi wa shule uliweka malengo yake ya kuborsha makazi ya walimu kwa kuanza kujenga nyumba tano ambazo mpaka sasa nyumba tatu zenye uwezo wa kuhifadhi walimu sita zimekamilika na nyingine moja mafundi wapo kazini na ya mwisho ikiwa hatua ya renta.
Hata hivyo Manga alimalizia kwa kutoa shukrani kwa mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas kwa mchango wake wa kimaendeleo ambao amekuwa akiufanya katika shule hiyo na mahali pengine.
Toa Maoni Yako:
0 comments: