Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Cheti cha Usajili wa Channel ya Utalii ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ya Tanzania Safari Channel baada ya kuzungumza na Kamati Maalum iliyoundwa na Serikali ya Uboreshaji wa Channel hiyo, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Januari 16, 2019.Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Ayoub Ryoba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Cheti cha Usajili wa Channel ya Utalii ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ya Tanzania Safari Channel baada ya kuzungumza na Kamati Maalum iliyoundwa na Serikali ya Uboreshaji wa Channel hiyo, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Januari 16, 2019. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji), Bibi Doroth Mwaluko, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazji Tanzania (TBC) William Kallaghe na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Ayoub Ryoba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru Katibu, Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji), Bibi Doroth Mwaluko (kushoto) wakati alipokabidhiwa Hati ya Usajili wa Channel ya Utalii ya TBC ya Tanzania Safari Channel katika kakao cha kuboresha Channel hiyo alichokiitisha, Ofisini kwake jijini Dodoma, Januri 16, 2019. Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), William Kallaghe na Watatu kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Ayoub Ryoba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati Maalum iliyoundwa na serikali ya kusimamia uboreshaji wa Channel ya Utalii ya TBC ya Tanzania Safari Channel, Ofisini kwa Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma Januari 16, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimazi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Meja Jenerali Mstaafu, Hamisi Semfuko baada ya kuzungumza na Kamati ya Maalum ya Uboreshaji wa Channel ya Utalii ya TBC ya Tanzania Safari Channel, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Januari 16, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea leseni ya usajili wa chaneli ya utalii ya Tanzania Safari ambayo itaiwezesha kuoneshwa kwa umma bila ya malipo yoyote (a must-carry channel) na wamiliki wa visimbusi.


Waziri Mkuu amekabidhiwa leseni hiyo leo mchana (Jumatano, 16 Januari, 2019) kwenye kikao alichokiitisha ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma ambako alitaka apewe mrejesho kutoka kwa wajumbe wa Kamati Maalum ya kusimamia uboreshaji wa Chaneli ya Utalii (Tanzania Safari Channel).

Akikabidhi leseni hiyo kwa Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayoub Rioba amesema kukamilika kwa usajili huo kumeiwezesha chaneli hiyo ianze kuonekana kwenye kisimbusi cha AZAM namba 109.

Akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Dkt. Rioba amesema Kamati hiyo iliundwa Desemba 21, mwaka jana na inajumuisha wajumbe kutoka taasisi ambata za maliasili na utalii kutoka Tanzania bara na Zanzibar.

“Baada ya kupata leseni, sasa hivi tunaonekana kwenye kisimbusi cha AZAM chaneli namba 109 na pia kwenye intelsat ambako tutaweza kuonekana kwenye nchi zote barani Afrika, sehemu kubwa ya bara la Ulaya na Uarabuni,” amesema.

Mapema, akichangia hoja kwenye kikao hicho, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA), Meja Jenerali (Mst.) Hamisi Semfuko alisema chaneli hiyo inaweza kunufaika kwa kupata matangazo kutoka kwa wamiliki wa mahoteli, makampuni ya kutoa huduma za utalii na wenye magari ya utalii.


Naye Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Dkt. Allan Kijazi alisema chaneli ya Tanzania Safari imekuja katika wakati muafaka kwa kuwa itaongeza juhudi za taasisi zao kutangaza vivutio vilivyopo nchini na hivyo kuongeza idadi ya watalii wa ndani na wa nje.


“Uwepo wa chaneli hii utasaidia kuondoa upotoshaji wa makusudi uliokuwa ukifanywa na baadhi ya nchi kuwa vivutio fulani viko kwenye maeneo yao wakati siyo kweli,” alisema.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: