Mwalimu Kandi S. Mbwambo akielezea kwa undani jambo fulani mbele ya washiriki wa semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) Mapema wiki hii, zinazofanyika kila jumatano katika ofisi za TGNP Mtandao zilizopo Mabibo jijini Dar es salaam .
Semina ikiendelea
Baadhi ya washiriki wakifuatilia semina kwa umakini.
Semina ikiendelea mapema wiki hii Makao Makuu ya TGNP Mtandao.


Inaeleweka kuwa unywaji wa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya, Lakini pia madhara mengine yatokanayo na unywaji wa pombe uliokithiri ni kusababisha ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.


Muwezeshaji wa semina Mwalimu Kandi Mbwambo akitoa ufafanuzi wa jambo kwa washiriki wa Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS).

Hayo yameelezwa mapema wiki hii na Mwalimu Kandi S. Mbwambo ambaye ni muwezeshaji kutoka Kituo cha Walimu Sinza (TRC) alipokuwa akiwasilisha mada inayosema ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kama matokeo ya unywaji pombe (ulevi).

Mwalimu Mbwambo alisema kuwa imezoeleka kuonekana kwa mzazi wa kiume akilewa pombe anakuja kuanzisha vurugu nyumbani kwa kupiga mke na watoto na jamii kumchukulia kama mlevi na kusahau kuwa kitendo hicho ni ukatili wa kijinsia.

Aidha aliendelea kusema kuwa ukiachia mbali vurugu lakini pia mlevi anaweza kutekeleza vitendo vingine visivyotarajiwa katika jamii kama kubaka na kulawiti watoto, kujikojolea na hata kutokwa na haja kubwa kwa wakati mwingine hali inayofanya heshima yake kushuka ndani ya jamii.

“Lakini pia kunywa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yake kwani anaweza kupata madhara ya kiafya ikiwemo kupata magonjwa kama TB, Mapafu kushindwa kufanya kazi kutokana na kunywa pombe kali, Na kwa muda mwingine hata kufanya ngono zembe hali inayoweza kusababisha kupata magonjwa ya zinaa ikiwemo Virusi Vya Ukimwi” alisema Mwalimu Mbwambo

Alisisitiza kuwa Mababa wengi wakishaanza unywaji wa pombe wanakuwa na matumizi makubwa ya pesa katika pombe na kusahau familia zao na wengine ufikia hata kutelekeza familia zao ama kukimbiwa na wenzi wao kutokana na kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.

Na baadhi ya wananchi walitoa maoni yao kuhusiana na nini kifanyike ili kupunguza madhara haya yatokanayo na pombe, Na wengi wao walisisitiza kuwa kupunguzwa kwa muda wa unywaji pombe ikiwezekana iwe ni kuanzia saa 12jioni mpka saa 2 usiku labda inaweza kusaidia.

“Lakini pia serikali kutekeleza sharia walizoziweka juu ya udhibiti wa Bar na pombe ili kuweza kuwepo na utulivu katika hili, kwa mfano kuviondoa vilabu holela vyote vinavouza pombe kinyume na sharia pamoja na kudhibiti uuzaji wa pombe kwenye maduka ya vyakula”. Walisema washiriki

Na mwisho walipendekeza elimu iendelee kutolewa kwa wananchi juu ya madhara ya pombe, pamoja na kutengeneza matangazo na kuyasambaza kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuhusu madhara ya unywaji wa pombe uliokithiri.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: