Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ali (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa jiji la Dodoma,Godwin Kunambi (kulia) alipotembelea shamba linalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) inayosimamia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na redio Uhuru,ikiwa ni mkakati wa kuanza uwekezaji wa ambapo kutajengwa mji wa kisasa pamoja na makao makuu ya ofisi za vyombo vya habari vya chama.
Mlinzi wa shamba hilo Zebeayo Lemgoha (kushoto) akimueleza jambo Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ali alipotembelea shamba linalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) inayosimamia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na redio Uhuru,ikiwa ni mkakati wa kuanza uwekezaji wa ambapo kutajengwa mji wa kisasa pamoja na makao makuu ya ofisi za vyombo vya habari vya chama.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ali ,akizungumza na Mlinzi wa shamba hilo Zebeayo Lemgoha (kushoto) ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma,Godwin Kunambi alipotembelea shamba linalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) inayosimamia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na redio Uhuru,ikiwa ni mkakati wa kuanza uwekezaji wa ambapo kutajengwa mji wa kisasa pamoja na makao makuu ya ofisi za vyombo vya habari vya chama
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ali (kulia) akimuonesha Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi walipofanya ziara ya kutembelea shamba linalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) inayosimamia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na redio Uhuru,ikiwa ni mkakati wa kuanza uwekezaji wa ambapo kutajengwa mji wa kisasa pamoja na makao makuu ya ofisi za vyombo vya habari vya chama
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ali akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kutembelea shamba linalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) inayosimamia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na redio Uhuru,ikiwa ni mkakati wa kuanza uwekezaji wa ambapo kutajengwa mji wa kisasa pamoja na makao makuu ya ofisi za vyombo vya habari vya chama
Mlinzi wa shamba hilo Zebeayo Lemgoha (kushoto) akionesha alama ya Shamba linapokomea kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ali aliye upande wa kulia huku mwaandishi wa Uhuru Gazeti pamoja na Mzalendo,Mussa Yusuph (katikati) akifatilia kwa makini maelezo yanayotolewa wakati wa ziara ya kutembelea shamba linalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) inayosimamia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na redio Uhuru,ikiwa ni mkakati wa kuanza uwekezaji wa ambapo kutajengwa mji wa kisasa pamoja na makao makuu ya ofisi za vyombo vya habari vya chama
Msimamizi Mkuu wa Vyombo vya Habari vya Chama, Ernest Sungura (katikati) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ali pamoja na Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi walipofanya ziara ya kutembelea shamba linalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) inayosimamia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na redio Uhuru,ikiwa ni mkakati wa kuanza uwekezaji wa ambapo kutajengwa mji wa kisasa pamoja na makao makuu ya ofisi za vyombo vya habari vya chama
Baada ya kumaliza kukagua shamba linalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) inayosimamia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na redio Uhuru,ikiwa ni mkakati wa kuanza uwekezaji wa ambapo kutajengwa mji wa kisasa pamoja na makao makuu ya ofisi za vyombo vya habari vya chama ,Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ali,akiwa na Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi wanamaliza ziara na kuanza safari ya kuondoka katika eneo hilo.
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi,akizungumza na waandishi wa habari hawapo (pichani) baada ya kumaliza ziara na atibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ali walipotembelea shamba linalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) inayosimamia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na redio Uhuru,ikiwa ni mkakati wa kuanza uwekezaji wa ambapo kutajengwa mji wa kisasa pamoja na makao makuu ya ofisi za vyombo vya habari vya chama PICHA ZOTE NA ALEX SONNA WA FULLSHANGWEBLOG, DODOMA.

Alex Sonna,Dodoma.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ali, ametembele shamba linalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) inayosimamia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na redio Uhuru, ikiwa ni mkakati wa kuanza uwekezaji wa ambapo kutajengwa mji wa kisasa pamoja na makao makuu ya ofisi za vyombo vya habari vya chama.

Dk. Bashiru aliambatana na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, Msimamizi Mkuu wa Vyombo vya Habari vya Chama, Ernest Sungura pamoja na baadhi ya wataalam wa mipango miji.

Katibu mkuu alisisitiza umuhimu wa vyombo hivyo kuhamia Dodoma kuunga mkono uamuzi wa waasisi wa taifa pamoja na ule wa Rais Dk. John Magufuli, wa kuhamishia makao makuu ya nchi kwenye mkoa huo.

"Nimekuja kuangalia eneo linalomilikiwa vyombo vya habari vya CCM kwa sababu sasa maeneo yanabadilika kuwa ya mipango miji. Tumekuja kuangalia usalama wa mipaka ili tuweze kupanga matumizi yake na vyombo vyetu viweze kuhamia Dodoma.

"Ni sehemu ya kuenzi mawazo na firka za viongozi, waasisi wa chama chetu na Baba wa taifa aliyeona mbali kwa kuichagua Dodoma kuwa Makao Makuu ya Chama na Serikali," Dk. Bashiru alisisitiza.

Hata hivyo amesema kuwa tayari maombi ya kubadilisha matumizi ya eneo hilo kutoka shamba hadi kutumika kwa shughuli za kibiashara au viwanda, yameshafikishwa kwenye Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji ambaye ndie mwenye jukumu la kusimamia sheria kwani chama hakipaswi kuwa sehemu ya kuvunja sheria.

"Kwa bahati nzuri nimelikuta shamba letu lipo salama limelindwa vizuri na tumeonyeshwa mipaka kitaalam. Wito wangu kwa wananchi wa Dodoma wanaotaka kuwekeza kwa kufanya shughuli za kibiashara au makazi, waheshimu sheria za mipango miji na ardhi," amesema Dk.Bashiru.

Aidha Dk. Bashiru alivitaka vyombo vinavyosimamia sheria vitende haki kwani maendelezo yote ya Jiji la Dodoma yanapaswa kufanyika kwa haki, amani na yawe kwa njia shirikishi.

"Naamini uongozi wa jiji na Serikali itazingatia misingi ya haki ili mipango miji ya Dodoma iwe ya mfano. Matarajio yetu ni kwamba usimamizi na utatuzi mzuri wa migogoro ya ardhi izingatie sheria na tusingepenga migogoro mingi ya ardhi kufikishwa mahakamani kwani inaweza kutatuliwa kwa njia za mazungumzo na kwa amani.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, amesema kuwa ziara ya Katibu mkuu kutembelea eneo linalomilikiwa na vyombo vya habari vya chama ni maandalizi ya awali kwa vyombo hivyo kuhama kutoka Dar es Salaam kuja Makao Makuu ya Nchi, Dodoma.

Kunambi amesema kuwa Katibu mkuu alikwenda kujiridhisha kwa namna gani anaweza kuzihimiza vyombo hivyo kuhamia Dodoma. Eneo lile lipo salama lakini maeneo yanayolizunguka yana migogoro mikubwa ya ardhi.

Kunambi alifafanua kuwa migogoro hiyo imegawanyika katika makundi manne ambapo kundi la kwanza ni la wakazi waliokutwa wakiishi kabla ya mwaka 1983 lilipopimwa kwa matumizi ya mashamba na wengine walimilikishwa baada ya upimaji mwaka 1983.

Alieleza kundi lingine ni la wavamizi waliongia kwenye maeneo hayo kwenye miaka ya 1990 ambao nao waliwauzia wengine ambao yatari wameshajenga makazi ya kudumu.

"Baada ya kubaini hili tumefanya mawasilianao na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kuomba kibali cha kubadili matumizi ya eneo lile kutoka mashamba hadi kuwa eneo la biashara, makazi na hoteli ili kutoa fursa kwa wananchi kuyaendeleza ambapo sasa tupo kwenye hatua za mwisho kuandaa ramani ya upimaji na mipango miji.

Mkurugenzi huyo wa jiji alifafanua hatua hiyo itasaidia kutatua migogoro iliyopo kwani vitapatikana viwanja vingi ambavyo makundi yote yatapata nafasi kwa kuzingatia sheria na taratibu za mipango miji.

Katika hatua nyingine Msimamizi Mkuu wa Vyombo vya Habari vya Chama, Ernest Sungura, amesema kuwa kazi iliyopo ni kuleta mageuzi makubwa kwenye vyombo vya habari vya chama kupitia kampuni ya Uhuru Media Group ambayo imeanza kwa mtindo wa kawaida wa kuboresha maudhui yaliyojikita kwenye ubora unaohitajika.

"UMG imejipanga kuwekeza na kuzalisha mapato yatakayotokana na huo uwekezaji ili tutumie uwekezaji huo na mapato kuvifanya vyombo vya habari vya chama viwe imara zaidi.

"Tumejipanga kuanzisha jiji la Uhuru Media. mipango ipo tayari tunafanya uwasilishaji kwenye vyombo hisika ndani ya chama na mara baada ya kukamilisha mchakato huo, tutaanza uwekezaji na hapo ndipo kutakuwa Makao Makuu ya Uhuru," Sungura, alibainisha.

Alieleza kuwa eneo hilo litakuwa na mitambo ya uchapaji, redio, televisheni, kumbi za mikutano, eneo la mafunzo ya namna ya kufundisha uendeshaji na usimamizi wa mikutano, biashara za hoteli na mahali ambako mandhari itabadilishwa kwa kuweka ziwa la kutengenezwa ili watu waweze kuburudika.

"Itakuwa aina ya Mlimani City iliyopo Dar es Salaam, ambayo sasa itakuwa Uhuru City iliyopo Dodoma. hilo ndilo jambo kubwa tunalokusudia kulifanya. Tutaanza mikakati ya kukusanya vyanzo vya mapato ili uwekezaji huo uanze mara moja.

Alisisitiza: "Mkakati utakuwa wa miaka 10 utakaofanyika kwa awamu ambapo tunataka tuache alama isiyofutika ndani ya miaka hiyo kwani tutakuwa na uwekezaji wa nguvu kwa ajili ya vyombo vya habari vya Uhuru.

Mlinzi wa shamba hilo Zebeayo Lemgoha,amesema kuwa amefurahishwa na viongozi wake kutembelea eneo hilo ambalo hadi sasa lipo salama na halijavamiwa. Eneo hili ni la kamapuni ya magazeti ya chama ambalo tangu mwaka 1992 nimekuwa nikililinda. Nitahakikisha litaendelea kuwa salama liweze kutumika kwa mipango iliyokusudiwa na chama chetu.

UMG kupitia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Redio Uhuru ipo kwenye maboresho makubwa kimaudhui na kimenejimenti ikiwa ni mkakati wa kuviimarisha zaidi vyombo vya habari vya chama kupitia Msimamizi Mkuu, Sungura.

Maboresho hayo yanahusisha mageuzi ya kimuundo na kimfumo ili vyombo hivyo vitoe ushindani madhubuti katika tasnia ya habari ndani na nje ya nchi pamoja na kuimarisha vyanzo vya mapato na kusaidia vyombo vya habari kujiendesha kama taasisi kamili zinazopata faida

Katika kipindi kifupi cha siku 100 tangu mkakati huo uanze kutekelezwa, tayari vyombo hivyo viimeanza kutoa ushindani mkubwa kwenye tasnia ya habari nchini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: