Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Mobisol Tanzania , Seth Matemu (wa pili kushoto) akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa hafla ya Kuadhimisha miaka 2 ya ushirikiano wa kibiashara kati ya Zuku Satellite Tanzania na Mobisol Tanzania . Kushoto ni Meneja Mauzo wa Zuku Satellite Tanzania, Nicolaus Kizenga ,Watatu ni Meneja Mkuu wa wa Zuku Satellite Tanzania, Thomas Wenanga, na Meneja Bidhaa wa Mobisol Tanzania, Lynda Okolo na Meneja Chapa kutoka Zuku.Veneranda Raphael.
Meneja Mauzo kutoka Zuku Satellite Tanzania, Nicolaus Kizenga( Kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari( hawapo pichani)kuhusiana na miaka miwili ya ushirikiano wa kampuni hiyo na Mobisol wa pili kushoto ni Mkuu wa Masoko wa Mobisol Tanzania, Seth Matemu ,Meneja Mkuu wa Zuku Satellite nchini Tanzania, Thomas Wenanga,Meneja Bidhaa wa Mobisol Tanzania, Lynda Okolo na Meneja chapa wa Zuku TV Veneranda Raphael.
Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Mobisol Tanzania, Seth Matemu ( wa pili Kushoto ) na Meneja Mkuu wa Zuku Satellite Tanzania, Thomas Wenanga, wakipongezana wakati wa hafla ya Kuadhimisha miaka 2 ya ushirikiano wa kibiashara wa kampuni hizo . ( Kushoto) ni Meneja Mauzo wa Zuku TV Tanzania, Nicolaus Kizenga, Meneja Bidhaa wa Mobisol Tanzania, Lynda Okolo na Meneja chapa wa Zuku TV , Veneranda Raphael (kulia).
Waandishi wa habari wakifuatilia matukio wakati wa mkutano huo
*Wananchi wafurahia umeme wa jua wa Mobisol na kuangalia Zuku TV
Makampuni ya Mobisol Tanzania na Zuku Satellite Tanzania, yameeleza dhamira ya kuendelea kuboresha maisha wa wakazi wa maeneo ambayo hayajafikiwa na umeme wa gridi ya taifa kupitia ushirikiano wake .
Mobisol imekuwa ikisambaza umeme wa jua maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji sambamba na kuuza vifaa vya kisasa vinavyotumia nishati hiyo, wakati kampuni ya Zuku Satellite Tanzania kupitia ushirikiano huu imekuwa ikiunganisha wateja wanaotumia umeme wa Mobisol na king’amuzi cha Zuku kwa vifurushi vya gharama nafuu vinavyowezesha kuona vipindi vya kielimu,burudani na michezo sambamba na kupatiwa vifaa na kupata huduma ya kufungiwa vifaa hivyo bure.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar e Salaam wakati wa kuadhimisha miaka miwili ya ushirikiano baina ya makampuni hayo, Mkuu wa Masoko wa Mobisol Tanzania,Bw.Seth Matemu, alisema “Tunajivunia kuendelea kuunganisha wateja katika umeme wetu sambamba na kuwapatia huduma ya vifaa bora vya kisasa vinavyotumia nishati hii.Tumeshirikiana na kampuni Zuku kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma mbalimbali wanazohitaji watumiaji wa umeme mahali popote wanapokuwa”.
Matemu ,alisema kuwa televisheni hivi sasa imekuwa zaidi ya kifaa cha kuleta furaha na burudani bali ni chombo cha kuelimisha pia kuwezesha kupata mapato kwenye maeneo ya mijini na vijijini,pia inatumika kwenye mabaa,migahawa,vituo vya sinema vijijini na kwa matumizi ya familia “Wakazi wa maeneo ya vijijini wanayo haki ya kupata taarifa na burudani kama wenzao wa mijini,wanastahili kupata burudani na kuishi maisha ya kisasa nasi tumejipanga kukidhi mahitaji yao”.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Zuku satellite Tanzania, Thomas Wenanga, alisema “Tunayo furaha kushirikiana na Mobisol kuweza kuwafikia watanzania kupata huduma ya kuona televisheni yetu ya kulipia ya Zuku.Katika kipindi cha miaka 2 ya ushirikiano tumepata mafanikio ya kuwafikia wananchi wanaoishi vijijini sambamba na kuwawezesha kupata burudani ya vipindi vyetu na tunawahakikishia wateja wetu kuwa tutaendelea kuwaletea mambo mazuri zaidi kupitia ushirikiano huu”.
Mobisol inawezesha kufunga umeme wa jua wenye nguvu ya 10 MW ambao umefikia kaya zaidi ya 500,000 katika ukanda wa Afrika Mashariki,pia inauza vifaa vya kisasa vinavyotumia nishati hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: