Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ndg. Japhet Justine akiungumza na viongozi wa wilaya ya Pangani wakati wa kikao chao cha pamoja kuhusiana ushirikiano
 Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah akizungumza katika kikao hicho kulia ni Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson George
 Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson George kulia akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ndg. Japhet Justine  kushoto akiangana na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
Wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kufanya mazungumzo hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mh. Zainab Abdalah ametembelea uongozi wa Benki ya Maendeleo ya kilimo nchini kufanya kikao kilichomkutanisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ndg. Japhet Justine na viongozi waandamizi ambao kwa pamoja wameahidi kuifanya Pangani wilaya ya mfano na ya kimkakati kwenye mipango yao.

Kikao hiki kimetoka na maazimio mazito kuelekea mapinduzi ya kilimo Pangani na moja kwa moja Mkurugenzi amekubali kua tayari kujenga kituo kikubwa cha ukusanyaji maziwa Pangani eneo la Madanga.

Aidha kikao kimeadhimia kuisaidia sekta ya uvuvi Pangani kuhakikisha inaleta mapinduzi ya uchumi kwa wavuvi.

Muhimu zaidi mazungumzo yamefanyika na kuweka misingi itakayowasaidia vijana wa Pangani hasa waliotayari kuungana na kunufaika na mipango ilioazimiwa na uongozi mzima kuahidi hivi karibuni kufika Pangani kuchagiza yaliopangwa na kujionea nini zaidi wanaweza kufanya na Pangani.

Mkuu wa Wilaya Pangani amemshukuru Kaimu Mkurugenzi Mtendaji kwa ufanisi wake na utayari aliounesha,kasi uwajibikaji na zaidi alivo tayari kujitoa kwa ajili ya Maendeleo ya nchi yetu. #Pangani&TADB #partnership #PanganiMpya
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: