Msanii Zaid na mwenzake wakiwa kwenye Jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea usiku wa kuamkia jana.
Msanii Lulu Diva akiwa kwenye Jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea usiku wa kuamkia jana.
Msanii Barnaba akiwa kwenye Jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea usiku wa kuamkia jana.
Msanii Mr Blue akiwa kwenye Jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea usiku wa kuamkia jana.
Msanii Fid Q akiwa kwenye Jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea usiku wa kuamkia jana.
Wasanii waliopanda jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote kwenye uwanja wa Majimaji Songea usiku wa kuamkia jana kwa pamoja wakiweka mishumaa juu kumkumbuka Mtayarishaji wa muziki Joshua Magawa a.k.a Pancho Latino aliyefariki hivi karibu kwenye kisiwa cha Mbudya jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Christina Mndeme akiongea na wananchi waliojitokeza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea usiku wa kuamkia jana.
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mhe.Pololite Mgema akiongea na wanachi waliojitokeza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea usiku wa kuamkia jana. Pembeni ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Christina Mndeme ns Mratibu wa Tamasha hilo Shafii Dauda.
---
Likiwa limeingia mkoa wanne Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote limefana na kuacha alama kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma usiku wa kuamkia jana, Kabla ya kuingia mkoani humo Tamasha hilo lililoanzia Mkoa wa Morogoro limepita mikoa ya Rukwa, Iringa, Songea na kuelekea Mtwara jumapili hii.
Akifungua Tamasha hilo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme aliyeongozana na mkuu wa wilaya ya Songea Mjini Mhe. Pololite Mgema alisema Tunawashukuru Kampuni ya Tigo na Clouds Media kwa kutuletea tamasha hili kubwa mkoani kwetu. “ Hii si kwa burudani pekee bali ni fursa kwa wakaazi wa mkoa huu kwa kuwawezesha kwa kuwaongezea kipato kwa kipindi hiki chote cha wiki nzima”. Niendelee kuwapongeza tena Tigo na Clouds Media na kuwaomba mwakani msiache kuja tena kwenye mkoa wetu.
Kwa upande wa burudani, ilianza kwa kumpata mshindi wa shindano la kusaka vipaji la Tigo Supa Nyota kwa kumuibua Msanii Single Baba atakayeiwakilisha Ruvuma kwenye fainali zitakazofanyika jijini Dar Es Salaam mwezi ujao.
Shoo rasmi ilianza kwa Msanii Mesen Selekta kufuatiwa na Rubby huyu ni msanii aliyeibuliwa kwenye Supa Nyota miaka kadhaa iliyopita, kwa kweli ni msanii wa aina yake aliweza kuteka hisia za mashabiki kwa kuimba nyimbo tofauti tofauti zikiwemo Niwaze,Ntade, Na Yule,Forever na nyingine.
Jumla ya wasanii kumi na mbili walipanda jukwaani wakiwemo Rostam, Weusi, Ruby, Mr. Blue, Barnaba, Zayd, Fid Q, Masen Selekta, Lulu Diva,Chege, Foby ambao wasanii hao ndio watapanda kwenye jukwaa jumapili uwanja wa Nangw’anda Mtwara.
Mdhamini mkuu wa msimu huu, kampuni ya Tigo imewakumbusha mashabiki wote wa muziki mjini Sumbawanga kufurahia promosheni zake tatu murwa katika msimu hii wa vibes. ‘Data Kama Lote inawapa wateja hadi mara mbili ya vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#. Hii itawawezesha wateja wa Tigo kufurahia msimu huu wa vibes kupitia mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+.
Huu ni mwaka wa 17 wa tamasha la muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ambapo mwaka huu linashirikisha 100% wasanii wa nyumbani watakaozuru mikoa 15 ya nchi ikiwemo; Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku kilele kikifanyika Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments: