Msanii Maua Sama akiwa kwenye jukwaa la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote usiku wa kuamkia Jumatatu tamasha lililofanyika kwenye uwanja wa Samora Mjini Iringa.
Umatu wa wakazi wa Iringa waliojitokeza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote usiku wa kuamkia Jumatatu tamasha lililofanyika kwenye uwanja wa Samora Mjini Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa , Richard Kasesela akilishwa keki na msanii Chege ambaye usiku wa Tigo Fiesta mjini Iringa ilikuwa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa , Richard Kasesela (mbele kulia) akicheza pamoja na wasanii waliotoa burudani kwenye Tamasha Kubwa la Tigo Fietsa 2018 Vibe Kama Lote uwanja wa Samora Mjini Iringa Usiku wa kuamkia jumatatu.
Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote 2018 limeendelea usiku wa kuamkia jumatatu kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa. Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa kampuni ya simu za mkononi Tigo kudhamini tamasha hilo.
Akizungumza mbele ya umati wa mashabiki waliohudhuria tamasha hilo Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini, Richard Kasesela amepongeza kampuni ya Tigo kwa kuwaletea burudani na fursa mbalimbali kwa wakazi wa Iringa. " Hii ni fursa ya pekee kwa wakazi wa mji huu ambayo kampuni ya Tigo imetuletea kwa mara nyingine ndani ya mkoa huu" Ukiondoa Burudani, pia wafanyabiashara wamenufaika sana ndani ya wiki nzima alisema Kasesela.
Pia mkuu huyo wa wilaya aliweza kupata nafasi ya kumkabidhi zawadi ya Keki kwa msanii Chege Chigunda kwa kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake.
Kwa upande wa Burudani wasanii wa kundi la Weusi ndio waliofunika kwenye tamasha hilo ilipopelekea mashabiki kuomba wasitoke kwenye jukwaa na kundi la Weusi walifanya hivyo hadi mwisho wa shoo kwa kuimba nyimbo zao nyingi za kuvutia zikiwemo, Madaraka,Swagire, NiCome na nyingine nyingi.
Mdhamini mkuu wa msimu huu, kampuni ya Tigo imewakumbusha mashabiki wote wa muziki kufurahia promosheni zake tatu murwa katika msimu hii wa vibes. ‘Data Kam Lote inawapa wateja hadi mara mbili ya vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#. Hii itawawezesha wateja wa Tigo kufurahia msimu huu wa vibes kupitia mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+.
Tigo pia inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Kwa Sumbawanga, tiketi zitakazonunuliwa kwa mfumo wa Tigo Pesa Masterpass QR zitagharimu TSH 5,000 pekee badala ya TSH 7,000 kwa watakaonunua kwa pesa taslim, Wateja wanapaswa kupiga *150*01# na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.
Wateja wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za kila wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia.
Toa Maoni Yako:
0 comments: