Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa, Bernard Makali (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo kuelekea Tamasha la Tigo Fiesta litakalofanyika siku ya Ijumaa mkoani humo, Wengine kwenye picha ni Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za Juu Kusini, Henry Kinabo (kushoto) na Msanii wa Bongo Fleva Nandy.
Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za Juu Kusini , Henry Kinabo akizungumza na waandishi wa habari leo kuelekea Tamasha la Tigo Fiesta litakalofanyika siku ya Ijumaa uwanja wa Nelson Mandela wilaya Sumbawanga. Wengine kwenye picha kulia ni Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa, Bernard Makali, Msanii Msanii wa Bongo Fleva Nandy na Mwisho kulia ni Katibu Tawala Msaidizi Idara ya Utawala, Winnie Kijazi na kushoto Msanii, Nikki wa Pili.
Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa, Bernard Makali (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wwafanyakazi wa Tigo na wasnii wataopanda leo kwenye jukwaa la Tigo Fiesta uwanja wa Nelson Mandela.
---
Baada ya mafanikio ya ufunguzi wa msimu wa Tigo Fiesta 2018- Vibe Kama Lote mjini Morogoro, sasa ni zamu ya Sumbawanga na viunga vyake kufurahia vibe lote katika msimu mkubwa zaidi wa muziki na utamaduni nchini uliowasili mjini hapo na promosheni tatu kabambe, fursa za kibiashara kwa wakaazi wote pamoja na ahadi ya vibes moto moto kutoka kwa 100% wasanii wa nyumbani.
Pazia la onesho hilo litakalofanyika katika viwanja vya Mandela mjini Sumbawanga litafunguliwa na wasaanii wanaochiopuka waliofanya vizuri katika shindano la kusaka vipaji la Tigo Fiesta 2018 – Supa Nyota. Wasanii wa kike Nandy na Maua Sama pia watakuwepo kukongo nyoyo za mashabiki, wakati wasanii wa hip-hop Fid Q, Bil Nas na kundi la Weusi linaloundwa na Joh Makini, Niki wa Pili pamoja na G-Nako nao watafunika onesho hilo. Mashabiki wa muziki pia wategemee kupata vibes za uhakika kutoka kwa wasanii wa bongo fleva Chegge, Jux, Whozu, Nedy Music, Barnaba na Marioo.
Mdhamini mkuu wa msimu huu, kampuni ya Tigo imewakumbusha mashabiki wote wa muziki mjini Sumbawanga kufurahia promosheni zake tatu murwa katika msimu hii wa vibes. ‘Data Kam Lote inawapa wateja hadi mara mbili ya vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#. Hii itawawezesha wateja wa Tigo kufurahia msimu huu wa vibes kupitia mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+,’ Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Kusini Henry Kinabo alisema.
Katibu Tawala mkoa wa Rukwa, Bernard Makali alielezea shukrani zake kwa waandaji kutoa fursa ya kuuitangaza wilaya hiyo akisema kuwa itaibua fursa nyingi zaidi za biashara na kujiongezea kipato kwa wakaazi.
Huu ni mwaka wa 17 wa tamasha la muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ambapo mwaka huu linashirikisha 100% wasanii wa nyumbani watakaozuru mikoa 15 ya nchi ikiwemo; Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku kilele kikifanyika Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments: