Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi Jumatano akifafanua jambo wakati kwenye kikao cha pamoja  mara baada ya kutembelea waendeshaji wa magazeti ya People's Daily  Online na China Daily nchini China kwa lengo la kujifunza na  kujadiliana namna bora zaidi ya kushirikiana katika sekta ya habari.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi sambamba na Ujumbe wake wakiwa kwenye kikao cha pamoja na baadhi ya Waendeshaji wa magazeti ya People's Daily Online na China  Daily nchini China kwa lengo la kujifunza na kujadiliana namna bora  zaidi ya kushirikiana katika sekta ya habari.
Baaadhi ya waendeshaji wa magazeti ya People's Daily Online na China Daily  nchini China wakifafanua jambo kwa wageni wao kutoka nchini Tanzania  (hawapo pichani) wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi,wakati wa kikao chao cha  pamoja na kuzungumza mambo mbalimbali kwa kwa lengo la kujifunza na  kujadiliana namna bora zaidi ya kushirikiana katika sekta ya habari.
Picha ya pamoja
Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi ( wanne kulia ) akiwa na ujumbe wake ambapo Jumatano Oktoba 24, 2018 walitembelea magazeti ya People's Daily Online na China Daily nchini China kwa lengo la kujifunza na kujadiliana namna  bora zaidi ya kushirikiana katika sekta ya habari.

Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, CHINA 

Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan  Abbasi Jumatano Oktoba 24, 2018 ametembelea magazeti ya People's Daily  Online na China Daily nchini China kwa lengo la kujifunza na  kujadiliana namna bora zaidi ya kushirikiana katika sekta ya habari. 

Akiwa katika vyombo hivyo, Dkt. Abbasi amesema kuwa China na Tanzania zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu kwenye masuala mbalimbali hivyo ni muda sasa wa kufanyia kazi mkataba wa ushirikiano wa Tanzania na China  kwenye masuala ya utamaduni na habari uliosainiwa mwaka 2016 

"Lengo la ziara yetu ni kujifunza wenzetu mnavyofanya kazi na pia kutafuta  namna ya kuweza kufanya kazi kwa pamoja katika sekta ya habari,"  ameongeza Dkt. Abbasi akiwa People's Daily. 

Amelitaka gazeti hilo  linalomilikiwa na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na linalofikisha habari zake kwa wasomaji milioni 700 duniani kupitia mitandao  mbalimbali kuenzi ushirikiano huo wa muda mrefu kwa kuzipa nafasi pia  habari za maendeleo za Afrika na Tanzania. 

Kwa upande wake  Meneja Mawasiliano wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Bw. Pascal Shelutete  amewakumbusha viongozi wa chombo hicho kuzipa fursa habari za utalii  hasa vivutio vingi vilivyoko Tanzania. Akiwa katika gazeti la China  Daily lililoanzishwa na Serikali ya China zaidi ya miongo mitatu  iliyopita, Dkt. Abbasi aliwaeleza wahariri wanaohusika na toleo maalum  la Afrika kuzingatia kuwa nchi nyingi za Afrika hasa Tanzania zina  maendeleo na vivutio vya uwekezaji vinavyopaswa kujulikana kwa wekezaji wengi wa China maombi ambayo wahariri wa gazeti hilo waliyakubali. 

Dkt. Abbasi anaendelea na ziara yake ambapo atatembelea television za China  za CCTV na CGTN na baadaye kufanya mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya  Redio China.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: