Diwani wa kata ya Idodi Onesmo Mtatifikolo ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa utoaji wa hati hizo katika kijiji cha Kitisi ambapo jamii ya wabarbaigi wanaishi maeneo hayo nao walipewa hati miliki za kimira na kuanza kukomesha hama hama ya kabili hilo la wafugaji
Wabarbaigi wanaoishi katika kijiji cha Kitisi kata ya Idodi wilaya ya Iringa wameanza kuondokana na mfumo dume baada ya kukubali wanawake kupatiwa hati miliki za kimila za maeneo ambayo wanamiliki mara baada ya kupata elimu kutoka mradi wa LTA wa feed the future
JAMII ya Wabarbaigi wanaoishi katika kijiji cha Kitisi kata ya Idodi wilaya ya Iringa wakiwa kwenye picha na viongozi mara baada ya kupatiwa hati miliki za kimila za maeneo ambayo wanamiliki mara baada ya kupata elimu kutoka mradi wa LTA wa feed the future
JAMII ya Wabarbaigi wanaoishi katika kijiji cha Kitisi kata ya Idodi wilaya ya Iringa wameanza kuondokana na mfumo dume baada ya kukubali wanawake kupatiwa hati miliki za kimila za maeneo ambayo wanamiliki mara baada ya kupata elimu kutoka mradi wa LTA wa feed the future unaotekelezwa katika wilaya za mkoa wa Iringa na Mbeya.
Wakizungumza wakati wa kukabidhiwa hati za kimira wanawake wa kibarbaigi walisema kuwa awali walikuwa hawaruhusiwi kumiliki mali yoyote ile bali mali zote zilikuwa zinamilikiwa na wanaume.
“Kwenye kabila letu mila zinawapa sana nafasi wanaume kumiliki mali na vitu vingine na kumfanya wanamke kuwa tegemezi jambo ambalo miaka ya nyuma limerudisha maendeleo nyuma ya wanawake” walisema wanawake hao wa Kibarbaigi
Wanawake hao walisema kuwa baada ya kupata elimu ya upimaji wa ardhi na kuifanya ardhi kuwa na hati miliki imesaidia wanaume wa kabila hilo kuanza kuitambua nafasi ya mwanamke na kumuwezesha mwanamke naye kumiliki mali sawa na wanaume wa kabila la wabarbaigi.
Tunaishukuru serikali na mradi wa LTA kwa elimu waliyoitoa kwa wanaume wa kabila la Barbaigi kwa kukubali wanawake wamiliki ardhi kwa kupewa hati miliki za kimira bila elimu hiyo wanawake sisi tungeendelea kuwa wakina mama wa nyumbani tu.
Naye mwenyekiti wa kabila hilo la wafugaji Shabani Ntasham alisema kuwa kupatikana kwa hati miliki za kimira kumekomesha hamahama ya jamii hiyo pamoja na kumuwezesha mwanamke wa jamii hiyo kumiliki ardhi.
“Sisi kabila letu ni watu wa kuhama hama hivyo baada ya kupata hati miliki za kimira sasa hatuwezi kuhama tena kwa kuwa tunamiki ardhi kisheria zinazotuwezesha kuboresha makazi yetu na kutufanya tuishi na kufanya shughuli zetu sehemu moja” alisema Ntasham
Ntasham alisema Mradi wa LTA wa feed the future unaofadhiwa na USD umetoa elimu kwa kabila la barbaigi na kusaidia kuanza kuondokana kwa kiasi chake mfumo dume kwa kuwawezesha wanaume wa kabila hilo kuwagawaia wanawake ardhi na kuzikatia hati miliki za kimila.
“Saizi umeona wanawake na wanaume wanafuraha kwa pamoja kwa kuwa kila mmoja anamiliki ardhi yake ambayo inamuwezesha kufanya jambo analolitaka kwa wakati wake tofauti kama ilivyokuwa hapo zamani” alisema Ntasham
Akizungumza na wanakijiji hao baada ya kukabidhi hati hizo diwani wa kata ya Idodi Onesmo Mtatifikolo alisema kuwa hati hizo zitawasaidia kutenga maeneo kwa ajili ya matumizi mbalimbali kwa kuzingatia uwezo wa ardhi kuhimili idadi hiyo na kasi ya ongezeko la watu na mifugo kwa miaka mingi ijayo.
Mtatifikolo aliongezea kuwa,hatua hiyo itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi kwa kuimarisha usalama wa miliki za ardhi na kuongeza thamani ambayo itawawezesha hata kukopesheka katika taasisi za kifedha zikiwemo benki.
“Usajili wa ardhi ni muhimu kwasababu unaongeza ulinzi wa umiliki wa ardhi, unawezesha uwekezaji, unaongeza thamani ya ardhi na unapunguza migogoro ya ardhi,” alisema Mtatifikolo
Aidha Mtatifikolo aliwaomba Feed The Future wautanue mradi huo angalau ufike umalize kupima vijiji vyote vya kata hiyo huku akivikumbusha vijiji vyote vya kata hiyo kuendelea kutoa ushirikiano kwenye miradi ambayo inasaidia kukuza maendeleo ya nchi.
“Tunataka katika kipindi ambacho Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) tuhakikishe tunapima ardhi na mipango ya matumizi bora na ipimwe ili kila mwenye kipande chake cha ardhi awe na hati yake,” alisema Mtatifikolo.
Mtatifikolo aliwataka wanakijiji wa kijiji hicho ambao hawajapimiwa maeneo yao kwa sababu mbalimbali ikiwemo ubishi na migogoro ya kifamilia kutumia vizuri muda ambao bado mradi huo upo katika wilaya hiyo na kuhakikisha nao wananufaika na zoezi hilo.
Awali naibu mkurugenzi wa Mradi wa LTA, Malaki Msigwa aliwapongeza wataalamu wa mradi huo kwa kuhakikisha wanawasaidia wananchi wa kijiji cha Kitisi kupima maeneo yao na kupata hati miliki za kimila ambazo zitakuwa msaada mkubwa kwenye maendeleo ya kiuchumi.
“Baadhi ya miradi imeibuliwa wakati wa upimaji wa ardhi hivyo ni fursa sasa kwa wananchi wenyewe kuitumia vizuri ardhi waliyopimiwa na kupewa hati miliki za kimila na kwa kuwa asilimia fulani kijiji hiki kimepimwa hivyo wanaweza kuwa kijiji cha mfano kwa kuwapa maendeleo hata wawekezaji wazuri kwa faida yao” alisema Msigwa
Toa Maoni Yako:
0 comments: