10. Congo DRC - Usd 3.4 Billion.
Taifa hili lilikuwa Taifa la kwanza kabisa kuingia Mikataba ya Mambo ya madini na Taifa la China.
09. GHANA - Usd 3.5 Billion.
Hali ya Ghana kiuchumi ni Mbaya kwa sasa kiasi kwamba imebidi wayakubali Masharti kadhaa ya IMF ili waweze kupewa Masaada wa pesa ili walipe deni la China.
08. NIGERIA - Usd 4.8 Billion
Kutakana na deni hili kuwakaba koo, Taifa hili kubwa la Afrika ya Magharibi sasa imebidi liikubali Shilingi ya China (Chinese Yen kutumika kama fedha ya kigeni katika Taifa lao - Foreign Currency)
07. CAMEROON - 5.5 Usd Billion
China imekubali kuwasamehe Cameroon sehemu ya Deni hili kwa masharti ambayo hayajawekwa hadharani.
06. ZAMBIA - 6.0 Usd Billion.
China imechukua Shirika la Umeme la Zambia kama Sehemu ya Malipo ya deni hili mara baada ya Zambia kushindwa kulipa...Republic of Zambia sasa unaweza kuiita "Repupuliki ofu Chambia"
05. SUDAN - 6.4 Usd Billion
Sudan kwa sasa wamepeleka Ombi maalumu huko China kuomba Msamaha wa Sehemu ya Deni,
04. CONGO BRAZAVILLE - 7.3 Usd Billion
Deni hili kwa sehemu kubwa Limesababishwa na Rushwa iuliyoshamiri nchini humo, fedha nyingi zimeliwa bila manufaa yoyote, Hali tete.
03. KENYA - 7.9 Usd Billion
Mabilioni haya mengi yalikopwa kwa ajili ya miradi ya miundo mbinu, lakini fedha nyingi zimeliwa na wajanja, Deni hili kubwa limechochewa hasa na Rushwa, Reli ya SGR kenya imejengwa kwa Gharama mara 4 zaidi ya Gharama za viwango vya kimataifa ..hata hivyo kenya imeongeza Ushuru wa Mafuta na bidhaa mbali mbali ili iweze kulipa deni hilo, na pia imeomba Msaada IMF na kuyakubali Masharti yao.
02. ETHIOPIA - 13.5 Usd Billion
Walikopa mapesa mengi kwa ajili ya maradi wa reli ya kutoka Ethiopia kwenda Djibouti, deni hili kubwa leo linawagharimu.
01. ANGOLA - 25 Usd Billion.
China wanaendelea kuchukua Mafuta kwa wingi huko Angola kama Sehemu ya malipo ya deni lao.
Toa Maoni Yako:
0 comments: