Benki ya CRDB yaahidi kuendelea kuwashika mkono shule za Marian kwa kutoa kiasi cha tsh milioni 5 ili ziweze kusaidia katika maendeleo ya shule hiyo.

Hayo ameyasema Meneja wa Tawi la Bagamoyo Bi. Nitike Nsekela wakati alipohudhuria katika mahafali ya kidato ya nne yaliyofanyika mjini Bagamoyo mjini.

Bi. Nitike amesema ni jukumu la jamii kwa ujumla kuungana katika malezi ya vijana na si kuachia majukumu walimu.

"Niwaombe wazazi tuungane pamoja katika malezi ya watoto wetu maana kipindi hiki cha utandawazi kinaharibu sana kizazi chetu, tuwe walinzi tusiwatupie majukumu walimu tu," amesema.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Bagamoyo mjini Bi. Nitike Nsekela ambaye alikuwa mgeni rasmi akitoa nasaha kwa wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Wasichana Marian wakati wa mahafali yaliyofanyika Bagamoyo-Pwani. Jumla ya wahitimu wapatao 113 wanatarajia kufanya mtihani wa Taifa kumaliza kidato cha nne 2018.
 Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Bagamoyo mjini Bi. Nitike Nsekela ambaye alikuwa mgeni rasmi akimkabidhi Mkuu wa shule ya Wasichana ya Marian ya Bagamoyo Mwalimu Martin Kakwezi hundi yenye thamani ya Tshs milioni 5 ikiwa ni mchango wao katika maendeleo ya shule hiyo.

Meneja Msaidizi wa Shule ya Wasichana ya Marian Padre Mugisha akitoa nasaha kwa wahitimu.

Mkuu wa shule ya Wasichana ya Marian ya Bagamoyo Mwalimu Martin Kakwezi akitoa wasifu wa shule yao.
  Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Bagamoyo mjini Bi. Nitike Nsekela ambaye alikuwa mgeni rasmi akiwakabidhi wanafunzi vyeti na zawadi zilizotolewa kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao.

Wahitimu wakifuatilia.

Wazazi waliohudhuria mahafali hayo.
Burudani toka kwa wanafunzi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: