Japokuwa serikali inajitahidi kuhakikisha nishati ya umeme inawafikia wananchi wote, imeelezwa kuwa wanawake wengi hasa wa vijijini hawanufaiki na nishati hiyo kwa kuwa shughuli nyingi za kiuchumi zinazofanywa na kundi hilo hazipewi nafasi ya kutumia nishati hiyo, hali inayofanya kuchelewa kwa maendeleo kutokana na matumizi ya zana hafifu kama mkaa na kuni.
Hayo yamesemwa mapema jana jijini Dar es salaam na Afisa kutoka Mtandao wa Jinsia na Nishati Tanzania Bw. Thabiti Mikidadi alipokuwa akiwasilisha mada katika semina ya kuwajengea uwezo wanachama wa Vituo vya Taarifa na Maarifa pamoja na wana Azaki mbalimbali zinazojihusisha na maswala ya nishati nchini.
Afisa kutoka Mtandao wa Jinsia na Nishati Tanzania Bw. Thabiti Mikidadi akiwasilisha hali halisi ilivyo kwa sasa nchini katika matumizi ya nishati mbadala.
Afisa huyo alisema kuwa mpaka leo wanawake wengi hasa wa vijijini wanashindwa kuzimudu gharama za nishati ya umeme na gesi na wanaendelea kutumia nishati ya mkaa na kuni japo kuwa inajulikana kuwa nishati hizo zina madhara makubwa kwa taifa na afya zao kwaujumla, inafahamika kuwa matumizi ya kuni yanawaharibu macho lakini pia mfumo wa upumuaji kwa kupata magonjwa kama TB na pia kukatwa kwa miti ovyo kunapunguza mvua na kusababisha nchi kuwa kame.
Aliendelea kusisitiza kuwa mwanamke anatumia muda mwingi sana kwa kwenda kutafuta kuni maporini lakini pia anaweza kukutana na madhara mbalimbali kama kubakwa, kudhurika na wanyama wakali na wakati mwingine hata kuuwawa.
Na mwisho walitoa rai kuwa wao kama wadau wa nishati na mazingira watajaribu kukaa pamoja na watunga sera ili kuona nini wafanye ili kupunguza tatizo hili na hatimaye ipatikane nishati mbadala kwa matumizi ya nyumbani hali itakayomfanya mwanamke awe salama katika shughuli zake za kila siku.
Mwanaharakati kutoka Kituo cha Taarifa na Maarifa Maganza Wilayani Kishapu Bw. Jerunga James akiwasilisha hali ilivyo katika kata yao mapema jana jijini Dar es salaam.
Kwa upande wake mwanaharakati kutoka Kituo cha Taarifa na Maarifa Maganza wilayani Kishapu bw. Jerunga James alisema kuwa serikali inatakiwa kuhakikisha umeme huu wa REA unaenea sehemu kubwa,
“kama kwetu kishapu hakuna nishati mbadala ya umeme wala gesi hivyo hali hii husababisha wanafunzi kutumia muda wa masomo na wengine kuzuiliwa na wazazi wao kwenda shule ili wakatafute na kwenda kuchanja kuni”. Alisema Jerunga
Aliendelea kusema kuwa wao kama wanaharakati kuhusiana na elimu walioipata leo watajaribu kushawishi serikali ya mtaa wao pamoja na kata katika mikutano ya kawaida na ya kuibua waweze kuingizia swala la elimu ya nishati mbadala ili walichokipata leo waweze kubadilishana uzoefu na wenzao ambao hawajapata nafasi hii.
Semina ikiendelea.
Toa Maoni Yako:
0 comments: