MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza katika mkutano wa wadau wa zao la korosho uliokuwa na lengo la kujadili maendeleo ya Tasnia ya zao la korosho kwa kipindi cha msimu wa miaka mitatu katikati ni Meneja Bodi ya korosho Kanda ya Kaskazini Mashariki Ugumba Kilasa na kulia ni Mrajisi Msaidizi vyama vya Ushirika Mkoa Tanga Jacklin Senzige
Meneja Bodi ya korosho Kanda ya Kaskazini Mashariki Ugumba Kilasa katika mkutano huo kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella.
MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Gwakisa Kasongwa katikati akiwa na wakuu wa wilaya wa wilaya za Kilindi Sauda Mtondoo kushoto kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa anayaafuata ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Mark wakifuatilia kwa umakini mkutano huo.
BODI ya korosho Mkoa Tanga imeshauriwa kuzitumia taasisi za Kijeshi za JKT Mgambo na JKT Maramba ili ziweze kusaidia katika mchakato wa uzalishaji wa miche ya mimea hiyo ya korosho.
Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa Mkoa Tanga Martin Shigella kwenye mkutano wa wadau wa zao la korosho uliokuwa na lengo la kujadili maendeleo ya Tasnia ya zao la korosho kwa kipindi cha msimu wa miaka mitatu.
Shigella alisema ili bodi hiyo iweza kukabiliana na uhaba wa miche katika Halmashauri zinazolima zao hilo lazima ifike wakati taasisi hizo ziweze kutumika kukabidhiwa mbegu kwa ajili ya kuzalisha miche hiyo.
“Jaribuni kuwasiliana na taasisi hizio za kijeshi ambazo wanawataalamu wa kuandaa vitalu wanaweza kuwasaidia kuzalisha miche mingi na iliyo na ubora unaotakiwa”Alisema Shigella.
Mbali na hilo pia alizitaka Halmashauri zote zinazolima zao hilo kuhakikisha zinatenga bajeti mapema ndani ya mwezi huu wa Sept kwa ajili ya ununuzi wa mbegu toka katika Taasisi ya Utafiti wa kilimo(Naliendele) kwa ajili ya uzalishaji wa miche ambayo inatarajiwa kusambazwa mwakani kwa wakulima wote
Toa Maoni Yako:
0 comments: