Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde akizungumza jambo wakati wa kufunga warsha ya Mashauriano kuhusu utekelezaji wa Sheria ya Baraza la vijana la Taifa iliyofanyika Agosti 1 na 2, 2018 Royal Village Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Asasi ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Vijana (YPC) Bw. Israel Ilunde akizungumza jambo na washiriki wa mkutano huo (kulia kwake) ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. Julius Tweneshi. (Wa kwanza kushoto) ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Asasi ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Vijana (YPC) Bw. Martin Mung’ong’o.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. Julius Tweneshi akizungumza na washiriki kutoka kwenye asasi mbalimbali za vijana walipokutana Jijini Dodoma, Agosti 2, 2018.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (wa pili kutoka kulia) akisikiliza lisara kutoka kwa Bi. Jane Mulungi wakati wa warsha hiyo iliyofanyika Jijini Dodoma. (Kushoto) ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Asasi ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Vijana (YPC) Bw. Martin Mung’ong’o, Mkurugenzi wa Asasi ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Vijana (YPC) Bw. Israel Ilunde. (Kulia) ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. Julius Tweneshi.
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (hayupo pichani) wakati wa warsha hiyo ya mashauriano kuhusu utekelezaji wa sheria ya Baraza la Vijana la Taifa.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia jambo lililokuwa linazungumzwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (hayupo pichani) walipokutana Jijini Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na viongozi wa Asasi ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Vijana (YPC) alipokutana nao jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (wa kwanza kulia) akiwa ameshika bendera ya Ushirikiano wa Ukanda wa Afrika Mashariki aliyokabidhiwa na viongozi wa asasi hizo za maendeleo ya vijana walipokutana Agosti 2, 2018 Jijini Dodoma. (Wa kwanza kushoto) ni Balozi wa asasi ya EAC, Bw. Evance Ayo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo mara baada ya kufunga rasmi warsha hiyo iliyofanyika Jijini Dodoma Agosti, 2018 (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU KAZI, VIJANA AJIRA NA WENYE ULEMAVU).
NA MWANDISHI WETU:
Serikali imeendelea kuwahakikishia vijana nchini kuhusu kushiriki kikamilifu katika kupanga na kutekeleza mipango mbalimbali ya kiuchumi na kijamii kwa maslahi ya kitaifa kwa ujumla.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde alipokutana na wadau kutoka asasi mbalimbali za vijana nchini wakati akifunga warsha iliyofanyika kwa siku mbili Agosti 1 hadi 2, 2018 iliyofanyika katika Hoteli ya Royal Village Jijini Dodoma.
Lengo la warsha hiyo ilihusu utekelezaji wa Sheria ya Baraza la Vijana la Taifa ambapo ilihusisha asasi mbalimbali za vijana ikiwemo Asasi ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Vijana (YPC), YUNA, TYVA, EAYT, TYC, Umoja wa Vijana CCM- Mkoa wa Dodoma na Baraza la Vijana CHADEMA – Mkoa wa Dodoma.
Waziri Mavunde alieleza kuwa Serikali inafahamu umuhimu wa Baraza la Vijana la Taifa, na hatua ya awali ya uundwaji wa kamati imeshakamilika ambapo itaanza kushughulikia uundwaji wa baraza hilo kuanzia ngazi ya chini hadi ngazi ya Taifa.
“Serikali itahakikishia vijana wanawezeshwa kiuchumi mahala popote walipo kupitia chombo hiko kitakachokuwa kinashughulikia masuala ya vijana na kuwasaidia kufikia malengo yao”
Aidha alitoa rai kwa vijana kutumia fursa ya uundwaji vikundi, makampuni au saccos kwa lengo la kukusanya mitaji itakayowafanya waweze kufikia mafanikio.
“Nitoe rai kwa vijana wote nchini ambao ndio nguvu kazi kubwa ya Taifa la Tanzania waunge mkono falsafa ya Serikali ya awamu ya tano kwa kushiriki kwenye uchumi wa viwanda kupitia Kilimo, Ufugaji, Uvuvi na shughuli mbalimbali za kiuchumi” alisisitiza Mavunde.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Vijana (YPC), Bw. Israel Ilunde aliongeza kuwa uanzishwaji wa sheria ya baraza la vijana utawanufaisha vijana wengi na mambo mbalimbali nchini.
“Niipongeze Serikali kwa hatua iliyofikia na iendelee kushirikiana na wadau pamoja na asasi hizi za vijana katika kutoa elimu na kuhamasisha vijana waweze kunufaika na adhima ya Serikali ya kuwaunganisha na kuwaletea vijana maendeleo” alisema Ilunde.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. Julius Tweneshi alieleza kuwa uundwaji wa baraza la vijana utaiwezesha Ofisi ya Waziri Mkuu hususan idara ya ajira kufanya kazi kwa karibu sana kama walezi, wasimamizi na waratibu wa taasisi zote za maendeleo ya vijana nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments: