Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dodoma kuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Mwezi wa Urithi linalotambulika kama ‘’Urithi Festival, Celebrating Our Heritage’’ litakalozinduliwa rasmi kitaifa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Septemba 15, 2018.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Urithi Festival walioshiriki kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari uliofanyika leo jijini Dodoma. Tamasha hilo linalotarajiwa kuzinduliwa Septemba 15, 2018 na  kuenzi, kudumisha, kuburudisha na kujifunza masuala muhimu yanayohusu Urithi wa Mtanzania hususani tamaduni zetu, historia, malikale na maliasili.
Baadhi ya Wajumbe wakiangalia nembo ya Urithi Festival inakayotumika kwenye Tamasha hilo. (Picha zote na Lusungu Helela-WMU)

NA LUSUNGU HELELA-DODOMA.

RAIS wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Mwezi wa Urithi linalotambulika kama Urithi Festival, Celebrating Our Heritage litakalozinduliwa rasmi kitaifa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Septemba 15, 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga amesema lengo la Tamasha hilo ni kuenzi, kudumisha, kuburudisha na kujifunza masuala muhimu yanayohusu Urithi wa Mtanzania hususani tamaduni zetu, historia, malikale na maliasili.

Aidha, Amesema kwa kutambua hazina kubwa ya malikale na utamaduni wa makabila zaidi ya 128 yaliyopo nchini, tamasha hilo litaongeza wigo wa mazao ya utalii kwa kukuza utalii wa utamaduni wa malikale hatua ambayo itaongeza ushindani wa Tanzania kama kituo bora cha utalii kwenye masoko mbalimbali duniani.

Ameongeza kuwa Urithi Festival itasadia kukuza utalii wa ndani kwa kuongeza muda wa watalii wa kimataifa kukaa nchini kwa vile Tamasha hilo lifanyika katika kipindi ambacho watalii wengi wanatembelea Tanzania.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: