Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mh.Jerry Muro amefanya ziara ya kushtukiza katika barabara ya mchepuko Arusha (Bypass) katika eneo la muungano Makumira na kubaini uwepo wa vitendo vinavyoashiria ukiukwaji wa taratibu za kazi na haswa katika kazi zinazofanywa na raia kutoka nje.
Mhe. Muro Pamoja nakuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo itakayosaidaia kupunguza msongamao wa magari kuelekea Jijini Arusha ameonyeshwa kukerwa na tabia ya baadhi ya wageni kufanya kazi zinazoweza kufanywa na watanzania jambo linaloendela kuminya fursa ya vijana wa kitanzaia kupata ajira.
Kutoka na sababu hiyo Dc Muro alilazimika kuchukua hatua ya kuwaagiza maofisa wa Uhamiaji kufuatilia suala hilo jambo lililopelekea kubainika uwepo wa RAIA Tisa ( 9 ) wa kigeni wanaofanya kazi hizo pasipo kuwepo na baadhi ya vibali husika vya kufanya kazi.
Katika ziara hiyo Dc Muro aliambatana na Naibu katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote ambao ni waratibu wa ujenzi wa Barabara hiyo.
Dc muro anaendelea na zoezi la ukaguzi wa miradi mbalimbali ya ujenzi katikaa wilaya ya Arumeru yenye kata 53 na Halmashauri mbili za Arusha Dc na Meru Dc.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: