Katibu Tawala wa wilaya ya Mkinga, Joseph Sura akizungumza namna walivyojipanga kuimarisha ulinzi mipakani kupitia vyombo vya ulinzi na usalama huku wakisisitiza hakuna ulazima wa kuvusha korosho nje ya nchi kwani athari zake ni kubwa
Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Tanzania,Bryson Mshana kulia akisistiza jambo kwa Katibu Tawala wa wilaya ya Mkinga (DAS) Joseph Sura kuhusu umuhimu wa matumizi sahihi na salama viwatilifu vinavyosambazwa na serikali kupitia na bodi ya korosho Tanzania lililoanza mikoa ya Mtwara na Lindi,Ruvuma na sasa Tanga watakwenda Pwani na mikoainayolima korosho
Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Tanzania, Bryson Mshana kushoto akisisitiza jambo na Nzaro Kijo ambaye ni Mratibu wa zao la Korosho Halmashauri ya wilaya ya Mkinga Abdallah Omari mwanakikundi akizungumza wamepata wafadhili kutoka Woldvision wamepata vifaa hivyo kwa ajili ya kubangulia korosho.
Mkazi wa Kijiji cha Gezani Kata ya Mkinga Hafidhi Mamboleo akiwa anapulizia dawa mikorosho
Sehemu ya viwatilifu vilivypo kwenye ghala la Mkinga
Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Tanzania, Bryson Mshana kulia akitoa elimu kwa wakulima wa zao la Korosho Kijiji cha Horohoro wilayani Mkinga kuhusu umuhimu wa matumizi sahihi nasalama viwatilifu vinavyosambazwa na serikali kupitia na bodi ya korosho Tanzania lililoanza mikoa ya Mtwara na Lindi,Ruvuma na sasa Tanga watakwenda Pwani na mikoa inayolima korosho,

KUTOKUWEPO kwa soko la uhakika wa zao la Korosho wilayani Mkinga mkoani Tanga kumepelekea baadhi ya wakulima kulazimika kuyasafirisha nchini Kenya kwa njia za panya kwa ajili ya kuuza ili waweze kupata fedha papo kwa papo badala ya kuuza kwa mfumo wa stakabadhi ghalani ambako wakati mwengine malipo yanachelewa kuwafikia.

Hayo yalibainishwa na Katibu wa Kikundi Kinachojushughulisha na Uzalishaji wa miche ya Korosho kilichopo Kijiji cha Horohoro kilichopo mpakani mwa Tanzania na Kenya (Kikohoki) Khalfan Mang’ana wakati wa zoezi la kutoa elimu kwa wakulima wa Korosho mkoa wa Tanga,juu ya matumizi sahihi na salama ya viwatilifu vya Mikorosho vinavyosambazwa na serikali kupitia Bodi ya Korosho Tanzania.

Alisema hali hiyo inatokana na wakati mwengine soko la kutokuwa zuri na kutokana na kuwa mpakani wanalazimika kuzisafirisha korosho zao tani kwa tani kwenda nchini Kenya ili kuweza kupata bei nzuri na soko ambalo linawawezesha kunufaika na kilimo hicho.

“Korosho nyingi tani kwa tani zinasafirishwa kwenda nchini Kenya kwasababu tupo mpakani ukienda ghalani unaambiwa kilo ni sh.2000 lakini kule nchini Kenya wananunua kilo 150 hadi 170 na ndio maana Korosho nyingi zinakwenda huko na hilo linatokana na kutokuwa kwa uzibiti wa bei hauridhishi “Alisema.

Naye kwa upande wake mkulima wa kukindi hicho Moni Rashidi alisema sababu kubwa ni kwamba wanapopeleka zao hilo nchini Kenya kuuza wanapata fedha papo kwa papo kuliko mfumo wa kupeleka ghalani ambapo wakati mwengine unaambiwa fedha zimechelewa jambo ambalo linekuwa likiwarudisha nyuma kimaendeleo.

Alisema licha ya hivyo wakati mwengine wanalazimika kuambiwa wachukue mizigo yao lakini iwapo bei hiyo itaboreshwa hawatakuwa na mpango wa kuzisafirisha kwani hata wenzao wa nchi hiyo wataileta nchini ili waweze kupata manufaa kupitia zao hilo.

Awali akizungumzia suala hilo la korosho kuvushwa nje ya nchi, Katibu Tawala wa wilaya ya Mkinga, Joseph Sura alisema kwanza wamejipanga kuwaelimisha wananchi kwamba bei iliyopo kutokana na soko letu ni nzuri na hakuna haja ya kuivusha nje ya nchi pasipo na ulazima.

Sura alisema pia wataimarisha ulinzi mipakani kupitia vyombo vya ulinzi na usalama huku wakisisitiza hakuna ulazima wa kuvusha korosho nje ya nchi kwani athari zake ni kubwa ikiwemo kuikosesha halmashauri mapato lakini pia fedha inayokwenda serikali kuu moja kwa moja kupitia bodi ya korosho inakosekana.

Hata hivyo alisema serikali imeweza kuagiza pembejeo na viwatilifu ambavyo vitapatikana kwenye wilaya hiyo hivyo ni fursa ikiwemo kwa wilaya nyengine kwa mkoa wa Tanga ili kuweza kupata mazao bora na kasi ya serikali kuhimiza korosho zao la biashara zinaloweza kuwakwamua kiuchumi.

Naye kwa upande wake, Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Tanzania,Bryson Mshana alisema zoezihilo linalofanyika kwa mkoa wa Tanga lina lengo la kutoa elimu ya matumizi sahihi na salama viwatilifu vinavyosambazwa na serikali kupitia na bodi ya korosho Tanzania lililoanza mikoa ya Mtwara na Lindi,Ruvuma na sasa Tanga watakwenda Pwani na mikoa inayolima korosho.

Alisema lengo ni wakulima kutambua viwatilifu vinavyosambazwa na serikali na vipo kwenye maeneo yao hivyo wanapaswa kufahamu namna gani wanaweza kuvipata kwa ajili ya kuvitumia.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: