Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipiga picha ya pamoja (Selfie) kwa kutumia simu yake ya mkononi na baadhi ya wafanyakazi wa Pori la Akiba Mpanga Kipengere alipotembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi. Nyuma yao ni Maporomoko ya Mto Kimani ambayo yana urefu wa mita 70, na ni chanzo kikuu cha maji yanayounda mto Ruaha hadi mto Rufiji.
Mbali na maporomoko hayo pori hilo pia lina wanyamapori mbalimbali ikiwemo Tumbili, Nyani, Tandala, jamii ya ndege mbalimbali ikiwemo wahamao kutoka ulaya wakati wa baridi kali na aina mbalimbali za maua ya asili ya kuvutia.
Dk. Kigwangalla amesema maporomoko hayo hayakuwahi kutumika ipasavyo kiutalii kutokana na kukosekana kwa miundombinu muhimu ikiwemo barabara ya kufika eneo hilo.
Amesema katika mwaka huu wa fedha Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kuboresha barabara hizo pamoja na kujenga ngazi kushuka kwenye kina cha maporomoko hayo hadi upande wa pili. Pori hilo pia lina kivutio cha pango alilojificha chief Mkwawa wakati wa vita ya pili ya dunia.
Kuna aina mbalimbali za utalii katika pori hilo ikiwemo utalii wa kupanda mlima, utalii wa kuogelea, utalii wa kutembea kwa miguu na utalii wa picha.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua shughuli za uhifadhi katika Pori la Akiba Mpanga Kipengere ambalo lipo katika wilaya za Mbarali (Mbeya), Makete na Wanging'ombe (Njombe) jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua shughuli za uhifadhi katika Pori la Akiba Mpanga Kipengere ambalo lipo katika wilaya za Mbarali (Mbeya), Makete na Wanging'ombe (Njombe) jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipiga jaramba wakati akikagua shughuli za uhifadhi katika Pori la Akiba Mpanga Kipengere ambalo lipo katika wilaya za Mbarali (Mbeya), Makete na Wanging'ombe (Njombe) jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa Maporomoko ya Mto Kimani (hayako pichani) na Meneja wa Pori la Akiba Mpanga Kipengere, Stanslaus Odhiambo alipotembelea pori hilo kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Makete mkoani Njombe jana. Maporomoko hayo yenye urefu wa mita 70 ni chanzo kikuu cha mto Ruaha Mkuu na Mdogo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa ramani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Mhifadhi Mkuu wa hifadhi hiyo, Dk. Chris Timbuka (wa pili kulia) alipotembelea bonde la Ihefu kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Mbeya jana. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Imani Nkuwi na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Mfaume.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa Maporomoko ya Mto Kimani na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Imani Nkuwi alipotembelea Pori la Akiba Mpanga Kipengere ambalo lipo katika wilaya za Mbarali (Mbeya), Makete na Wanging'ombe (Njombe). Maporomoko hayo yenye urefu wa mita 70 ni chanzo kikuu cha mto Ruaha Mkuu na Mdogo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Wawindi iliyopo wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo iliyofadhiliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) shuleni hapo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Igaza iliyopo wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo iliyofadhiliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) shuleni hapo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: