ZAIDI ya Sh.milioni 46 kutoka Mfuko wa Jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto, Mkoani Tanga zimegawiwa kwenye kata 18 za jimbo hilo ili kuweza kuchangia kasi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Bumbuli ni Jimbo linaloongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulia Mazingira na Muungano January Makamba.
Kwa mujibu wa Katibu wa Mbunge wa Jimbo hilo, Hozza Mandia alitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na miradi ya huduma ya maji, ujenzi wa madarasa, zahanati na matengenezo ya barabara.
Mandia alitaja mchanganuo wa pesa hizo zilizotolewa kuwa kata ya Kisiwani imepata jumla ya sh. Milioni 4 kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa mradi wa huduma ya maji, wakati ambapo kata ya Tamota itapatiwa Sh. Million 3 kwa ajili ya ujenzi wa zahanatati katika kijiji cha Ngwelo.
Miradi mingine ni mradi wa zahanati katika kijiji cha Tekwa ambao mfuko umechangia Sh. Milioni 1.44, mradi wa zahanati kwemsambia aruji yenye thamani ya Sh 675,000, saruji ye thamani kama hiyo kwa mradi wa ujenzi wa darasa shule ya msingiya kivilu na saruji nyingine yenye thamani sh. 700,000 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa ofisi ya kata ya Kwemkomole.
Kata ya Dule B itapata mchango wa jumla ya Sh. Milioni 3.42 milioni kwa ajili ya miradi mbalimbali, , wakati ambapo kata ya Mamba imepata jumla ya Sh. Milioni 3.4, Bumbuli (Sh. 2.99 milioni), Vuga (Sh. 2.97 milioni) na Mponde (Sh. 2.25 million).
Diwani wa Kata ya Vuga Jumaa Dhahabu alisema kuwa fedha hizo zitawasaidia kuweka lenta kwenye jengo la zahanati pamoja na kuweka sakafu kwenye chumba cha darasa kinacho tumika kwaajili ya maabara ya sayansi na kuweka miundombi katika darasa mabara hiyo ameongeza kwa kusema anamshukuru Mbunge wa Jimbo hilo kwanamna anavyoendelea kuwasaidia katiaka kata ya vuga
Hata hivyo alisema kuwa serikali iliwapatia sh. Million 10 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya kata ya kwemkomole , hivyo fedha hizo zitawasaidia kusafisha jengo hilo nakwamba kama viongozi wa kata hiyo tayari wamepokea mifuko 200 ya saruji kutoka kwa Mbunge wa jimbo hilo January Makamba ambayo itapelekwa kwenye madarasa naa zahanati .
Toa Maoni Yako:
0 comments: