Mashabiki wa Timu ya Japan wakifanya usafi uwanjani mara baada ya mechi kumalizika.
Mashabiki wa Timu ya Japan wakifanya usafi uwanjani mara baada ya mechi kumalizika.
Shirikisho la soka duniani limekoshwa na ustaarabu wa mashabiki na wachezaji wa timu ya taifa ya Japan ambao baada ya mchezo wao wa jana dhidi ya Ubeligiji ambao uliisha kwa wao kufungwa 3-2, walianza kazi ya kuusafisha uwanja kwa kuokota takataka zote uwanjani na usafi wa kina katika chumba chao cha kubadilishia nguo.

‘Ni jambo zuri na la kukumbukwa kwa muda wote ‘ alisema msimamizi wa kituo.

Katika vyumba vya kubadilishia wachezaji na viongozi wa timu hiyo walifanya usafi wa kina na kuacha ujumbe mezani ‘Asante Urusi'.

Mara nyingi katika soka timu inayofungwa katika michuano mikubwa yenye masilahi mapana kama hii ya kombe la Dunia huamsha uchungu na hasira kwa mashabiki na wachezaji ambao mara nyingi huishia katika uharibu wa mali na miundo mbinu au ugomvi lakini Wajapani wameonesha nidhamu kubwa, upendo na heshima katika mchezo wa soka.

Wenyeji wa michuano hiyo Warusi wameliona tukio hilo kama heshima kwao na kujali mchango wao wa kuandaa michuano hiyo. Shirikisho la soka nchini Urusi tayari limetuma ujumbe wao wa shukrani kwa wenzao wa Japan kwa ukarimu wao mkubwa walionesha kwa usafi wa Uwanja na ujumbe wa shukrani.

N:B
Tuache kung’oa viti tukifungwa tuwaige wajapani na ustaarabu wao
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: