
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Véron Mosengo-Omba, ametangaza kujiuzulu wadhifa wake baada ya zaidi ya miaka 30 ya utumishi katika soka la kimataifa.
Katika taarifa rasmi iliyotolewa jijini Cairo Machi 29, 2026, Mosengo-Omba amesema amefikia uamuzi huo ili kujikita katika miradi binafsi baada ya kujitolea kwa muda mrefu kukuza soka kama chombo cha kuunganisha watu, kutoa elimu na kuleta matumaini.
Amesema kuwa sasa anaondoka akiwa na amani ya moyo baada ya kuondoa tuhuma zilizokuwa zikimkabili, akibainisha kuwa anaiacha CAF ikiwa imara zaidi na yenye mafanikio makubwa kuliko ilivyokuwa awali.
Mosengo-Omba pia alimshukuru Rais wa CAF, Patrice Motsepe, pamoja na timu yake na wadau wote wa soka barani Afrika kwa ushirikiano wao uliochangia mafanikio ya maendeleo ya mchezo huo.
Amehitimisha kwa kueleza matumaini yake kuwa mafanikio yaliyopatikana ndani ya CAF yataendelea kudumu na kuimarika zaidi katika siku zijazo.
Moshi ilichangamka kwa mara nyingine tena huku maelfu ya wakimbiaji, mashabiki, na watazamaji wakikusanyika kwa toleo la mwaka 2026 la Kilimanjaro Marathon. Kilichoanza zaidi ya miongo miwili iliyopita kama mbio, kimekua na kuwa moja ya majukwaa yenye nguvu zaidi kitaifa nchini Tanzania, yakileta pamoja michezo, utalii, utamaduni, na jamii kwa namna ya kipekee.
Mbio za mwaka huu zilivutia ushiriki mkubwa kutoka kote Tanzania na duniani kwa ujumla, na kuimarisha nafasi yake kama tukio muhimu la utalii wa michezo. Kuanzia wanariadha wa kiwango cha juu hadi wakimbiaji wa mara ya kwanza, tukio hili liliunda uzoefu wa pamoja uliovuka mstari wa mwisho wa mashindano. Haikuwa tu kuhusu ushindani, bali pia ushiriki, muunganiko, na fahari ya taifa.
Afya na ustawi pia vinaendelea kuwa sehemu muhimu ya faida ya marathon hii. Kwa miaka mingi, tukio hili limechangia kujenga utamaduni wa kukimbia na kuishi maisha yenye afya nchini. Watu wengi zaidi wanashiriki katika shughuli za mazoezi, na taasisi mbalimbali zinaanzisha majukwaa yanayohamasisha harakati na ustawi wa mwili. Marathon imekuwa mfano wa kile ambacho juhudi endelevu za afya ya jamii zinaweza kufanikisha nchini Tanzania.
Burudani haikuishia kwenye mbio pekee. Kili Dome kwa mara nyingine ilileta pamoja michezo, muziki, sherehe, na kuunda mazingira yenye hamasa ambapo washiriki na watazamaji waliweza kuungana na kujiburudisha. Mchanganyiko huu wa michezo na maisha ya kijamii unaakisi nafasi pana ya marathon katika kuunda uzoefu wa pamoja.
Akizungumza baada ya tukio, Mkurugenzi Mtendaji Michelle Kilpin alieleza ukuaji na umuhimu unaoendelea wa marathon hii kama jukwaa la kitaifa.
“Marathon ya Kilimanjaro inaendelea kuwaleta watu pamoja kutoka asili mbalimbali kwa namna inayoakisi maana halisi ya Tanzania. Inaunga mkono utalii, inakuza afya, na inajenga mahusiano yenye maana katika jamii. Tunajivunia kuona jinsi tukio hili linavyoendelea kukua na kutoa thamani zaidi ya mbio zenyewe.”
Kadri toleo la mwaka 2026 linavyohitimishwa, Kilimanjaro Marathon inabaki kuwa zaidi ya tukio la kila mwaka la michezo. Ni jukwaa linalochochea shughuli za kiuchumi, linaimarisha mshikamano wa jamii, linahamasisha maisha yenye afya, na linaonesha Tanzania kwa dunia.
Kupitia uungwaji mkono wake unaoendelea, Tanzania Breweries Plc kupitia Kilimanjaro Lager inaendeleza dhamira yake ya kusaidia mipango inayowaunganisha watu na kuchangia maendeleo ya muda mrefu ya taifa. Mbio zinaweza kuishia kwenye mstari wa mwisho, lakini faida yake inaendelea kwa muda mrefu zaidi.
Na Mwandishi Wetu.
Dar es Salaam — Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetoa adhabu mbalimbali kwa klabu na waamuzi kufuatia matukio ya kinidhamu yaliyojitokeza katika michezo ya Ligi Kuu ya NBC, ikiwemo kuifungia mchezaji wa Young Africans, Djigui Diarra, na kuipiga faini klabu ya Simba SC.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na TPLB, Diarra amefungiwa mechi tatu pamoja na kutozwa faini ya Sh milioni 2 baada ya kumshambulia mwamuzi kufuatia mchezo kati ya Mtibwa Sugar na Young Africans uliomalizika kwa sare ya 1-1 katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Aidha, mchezaji huyo pia ametozwa faini nyingine ya Sh milioni 2 kwa kosa la kuonesha ishara isiyo ya kiungwana kwa mwamuzi baada ya kumalizika kwa mchezo huo.
Katika hatua nyingine, klabu ya Simba SC imetozwa faini ya Sh milioni 10 baada ya mashabiki wake kuwarushia waamuzi chupa za maji walipokuwa wakitoka uwanjani kufuatia mchezo dhidi ya Pamba Jiji FC uliomalizika kwa sare ya 1-1. Tukio hilo limetajwa kuwa ni la kujirudia ndani ya kipindi kifupi.
Kwa upande wa klabu ya TRA United, nayo imetozwa faini ya Sh laki tano baada ya wachezaji wake kuonyeshwa kadi zaidi ya tano katika mchezo mmoja dhidi ya Young Africans, hali inayokiuka kanuni za nidhamu za ligi.
Sambamba na adhabu hizo, TPLB pia imewachukulia hatua baadhi ya waamuzi wa mechi husika. Mwamuzi wa kati, Gilbert Mrina, ameshushwa daraja kwa kushindwa kuchukua hatua stahiki kwa kosa la kinidhamu lililofanywa na mchezaji Diarra, huku mwamuzi msaidizi Abdulaziz Ally akifungiwa mechi tano kwa kushindwa kutafsiri vyema sheria ya mpira wa miguu katika tukio la kuotea.
TPLB imesisitiza kuwa hatua hizo zimechukuliwa kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu ili kuhakikisha nidhamu, haki na uwazi vinaendelea kudumishwa katika mashindano hayo.
Klabu ya Simba SC imefanikiwa kumbakisha kiungo wake mahiri, Elie Mpanzu, baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuitumikia timu hiyo.
Hatua hiyo imepokelewa kwa furaha kubwa na mashabiki wa klabu hiyo, wakieleza kuwa kuendelea kubaki kwa nyota huyo wa kimataifa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni faraja kubwa kuelekea misimu ijayo.
Wadau wa soka nchini pia wamempongeza Rais wa klabu hiyo, Mohammed Dewji, kwa juhudi zake katika kuhakikisha mchezaji huyo muhimu anaendelea kubaki ndani ya kikosi hicho.
Mpanzu amekuwa miongoni mwa wachezaji tegemeo ndani ya Simba SC, akionesha kiwango cha juu katika safu ya kiungo na kuchangia mafanikio ya timu hiyo katika mashindano ya ndani na kimataifa.

Uongozi wa Simba umeeleza kuwa kuendelea kumbakisha mchezaji huyo ni sehemu ya mkakati wa kuijenga timu imara itakayoweza kushindana katika ngazi ya juu zaidi, ikiwemo mashindano ya kimataifa barani Afrika.Kwa upande wao, mashabiki wameonesha matumaini kuwa uwepo wa Mpanzu utaongeza nguvu katika kikosi hicho na kusaidia timu kufikia malengo yake ya kutwaa mataji makubwa msimu ujao.
Kuongezwa kwa mkataba huo ni ishara ya dhamira ya Simba SC kuendelea kuwekeza kwa wachezaji bora na kudumisha ushindani katika soka la Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves, beki huyo alipata majeraha ya kifundo cha mguu wakati wa mchezo wa dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba S.C. uliochezwa mapema mwezi Machi 2026. Kutokana na majeraha hayo, Job alilazimika kutolewa uwanjani mapema na nafasi yake kuchukuliwa na beki mwingine.
Kocha huyo amesema majeraha hayo yatamfanya mchezaji huyo kukosekana katika michezo kadhaa ya Ligi Kuu Tanzania Bara huku akipatiwa matibabu na uangalizi wa karibu na madaktari wa klabu hiyo.
Dickson Job ambaye ni mmoja wa mabeki tegemeo wa Yanga na Taifa Stars, ameendelea kuwa mhimili muhimu katika safu ya ulinzi ya timu hiyo tangu alipojiunga akitokea Mtibwa Sugar F.C. mwaka 2021.
Kutokana na hali hiyo, benchi la ufundi la Yanga linatarajiwa kutumia mabeki wengine kuziba pengo lake hadi atakapopona na kurejea uwanjani.

Na Mwandishi Wetu
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu, FIFA, limethibitisha rasmi ushiriki wa Nigeria katika mashindano ya FIFAe Nations League 2026, hatua inayotajwa kuimarisha nafasi ya taifa hilo katika ulimwengu wa michezo ya kielektroniki (esports).
Kwa mujibu wa taarifa ya FIFA, mashindano ya msimu ujao yatahusisha mikondo mitatu ambayo ni eFootball ya console, eFootball ya simu, pamoja na Rocket League. Takwimu zinaonesha kuwa jumla ya nchi 115 zimefuzu katika kundi la console, 81 katika mobile na 84 katika Rocket League, huku Nigeria ikifanikiwa kufuzu katika makundi yote matatu.
Ushiriki huo unalipa taifa hilo fursa mpya ya kujipambanua kimataifa baada ya kushindwa kufika mbali katika Kombe la Dunia la FIFAe 2025 lililofanyika Saudi Arabia, ambapo timu ya Nigeria ilitolewa hatua ya robo fainali baada ya kufungwa na Afrika Kusini.
Wakati huohuo, macho ya wadau wa soka bado yanaelekezwa kwa uamuzi unaotarajiwa kutolewa na FIFA kuhusu rufaa iliyowasilishwa na Nigeria Football Federation dhidi ya Fédération Congolaise de Football Association kuhusiana na madai ya uhalali wa mchezaji katika mchezo wa mtoano wa kufuzu Kombe la Dunia 2026.
Katika mchezo huo, DR Congo ilisonga mbele kwa ushindi wa mikwaju ya penalti na kufuzu hatua ya mtoano wa kimataifa, lakini iwapo FIFA itaamua kuipatia haki Nigeria, timu ya taifa ya nchi hiyo, Super Eagles, inaweza kurejeshwa katika hatua hiyo.
Hata hivyo, kwa sasa uthibitisho wa ushiriki wa Nigeria katika FIFAe Nations League unaonekana kuwa faraja kubwa na hatua muhimu katika kukuza ndoto za taifa hilo ndani ya sekta inayokua kwa kasi ya esports duniani.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya klabu iliyotolewa Februari 27, 2026, Aucho amepewa adhabu ya kusimamishwa kazi kwa miezi mitatu kutokana na tuhuma za utovu wa nidhamu na ukiukwaji wa majukumu ya kazi. Naye kipa Amas Obasogie amesimamishwa kwa muda huo huo wakati uchunguzi ukiendelea kuhusu tuhuma za upangaji wa matokeo.
Klabu hiyo imesisitiza kuwa hatua hizo zimechukuliwa kulinda misingi ya nidhamu, uwajibikaji na heshima ndani ya timu, huku ikiwataka wachezaji na watumishi wote kuzingatia maadili ya kazi.
Wakati huo huo, Aucho ameonekana kujibu hali hiyo kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, akieleza kuwa katika maisha yake yote ya soka amekuwa akijituma kwa weledi, heshima na nidhamu kwa kila klabu aliyowahi kuitumikia. Amesisitiza kuwa hajawahi kuhusishwa na tukio lolote la utovu wa nidhamu, akibainisha kuwa anaelewa wajibu mkubwa unaokuja na taaluma ya soka la kulipwa.
Aidha, aliwashukuru mashabiki wake kwa kuendelea kumuunga mkono katika kipindi hiki, akisema anaamini hali ya sasa itapita na ataendelea kusimama imara katika taaluma yake.

Mashindano ya vijana ya mchezo wa Tanzanite Junior Chess Championship yanatarajiwa kufanyika Aprili 4 na 5, 2026 katika jiji la Dar es Salaam, yakilenga kukuza vipaji vya watoto na vijana katika mchezo huo wa kimkakati.
Mashindano hayo yatawakutanisha washiriki kutoka makundi mbalimbali ya umri kuanzia chini ya miaka sita hadi chini ya miaka 20, ambapo kila mshiriki atacheza raundi sita zenye dakika 25 kwa kila mchezaji. Waandaaji wamesema tukio hilo linalenga kujenga uwezo wa kufikiri, nidhamu na ubunifu miongoni mwa vijana.
Mbali na ushindani, washindi watapata vikombe, medali pamoja na vyeti vya ushiriki, hatua inayotarajiwa kuwahamasisha vijana wengi zaidi kujihusisha na mchezo wa chess nchini.
Kaulimbiu ya mashindano hayo ni “Smart Moves, Bright Futures,” ikisisitiza umuhimu wa maamuzi sahihi katika kujenga mustakabali bora kwa kizazi kijacho. Waandaaji wamewahimiza wazazi, shule na wadau wa michezo kuhamasisha watoto kushiriki ili kukuza vipaji na kuimarisha michezo ya kiakili nchini.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Makongoro Nyerere, amempongeza mwanawe Prince Nyerere pamoja na mjukuu wake Charles baada ya kutwaa tuzo ya ARC2 katika mashindano ya FIA African Rally Championship.
Kupitia ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Nyerere alisema amefarijika na kujivunia mafanikio ya vijana hao, akieleza kuwa ni Watanzania wa kwanza kushinda tuzo hiyo katika zaidi ya miaka 45 ya mashindano hayo.

Aliongeza kuwa ushindi huo ni ushahidi kuwa nidhamu, bidii na uzalendo vinaweza kuzaa matokeo makubwa, huku akisisitiza kuwa mafanikio hayo yanaipa heshima familia na taifa kwa ujumla.

Vijana hao walitunukiwa tuzo hiyo Februari 15, 2026 katika hafla ya Tanzania National Motorsports Awards, hatua inayochukuliwa kama mafanikio makubwa kwa michezo ya magari nchini.
Mwanariadha nyota wa Tanzania, Gabriel Geay, ameshinda mbio za Daegu Marathon za mwaka 2026 kwa muda wa saa 2:08:09, akifanikiwa kutetea ubingwa wake wa mwaka uliopita.
Katika ushindani huo mkali, jukwaa la washindi (podium) lilishuhudia historia ya kipekee baada ya Watanzania wawili kuingia katika tatu bora:
Matokeo ya Juu – Wanaume
Gabriel Geay (🇹🇿) – 2:08:09
Chimdesa Gudeta (🇪🇹) – 2:08:09
Josphat Gisemo (🇹🇿) – 2:08:17
Tukio hilo limeacha gumzo kubwa kwenye mbio za kimataifa baada ya Tanzania kupata wawakilishi wawili kwenye tatu bora huku hakuna mwanariadha kutoka Kenya aliyeingia kwenye tano bora.
Mkenya wa kwanza kumaliza mbio hizo alikuwa Stanley Bett, aliyeshika nafasi ya sita kwa muda wa 2:10:31.
Ushindi huo unaendelea kuimarisha hadhi ya Tanzania katika mbio za masafa marefu duniani na kuthibitisha kuwa taifa hilo linaendelea kuzalisha wakimbiaji wa kiwango cha juu.
Na Mwandishi Wetu.
Matumaini ya timu ya taifa ya Nigeria, Super Eagles, kufuzu Kombe la Dunia 2026 yamepata msukumo mpya kufuatia shinikizo linaloendelea ndani ya uongozi wa Shirikisho la Soka Afrika, CAF.
Hali hiyo inakuja wakati Nigeria ikiendelea kusubiri uamuzi wa Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, kuhusu malalamiko yao dhidi ya timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DR Congo, kwa madai ya kutumia wachezaji wasioruhusiwa katika mechi ya mchujo wa Afrika.
Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) liliwasilisha malalamiko hayo Desemba mwaka jana likidai kuwa DR Congo huenda ilitumia hadi wachezaji sita wenye dosari katika vibali vyao wakati wa fainali ya mchujo iliyochezwa nchini Morocco. Katika mchezo huo, Nigeria ilipoteza kwa penalti 4-3, matokeo yaliyozima ndoto zao za kufuzu moja kwa moja hatua ya mchujo wa mabara.
Hata hivyo, hali mpya imejitokeza baada ya Rais wa Chama cha Soka cha Mauritius, Samir Sobha, kumtaka kuondolewa kwa Katibu Mkuu wa CAF, Véron Mosengo-Omba, akidai hana mamlaka ya kisheria kuendelea kushika wadhifa huo. Mosengo-Omba anatoka DR Congo, jambo ambalo baadhi ya wadau wanaamini linaweza kuibua mgongano wa maslahi katika kushughulikia malalamiko ya Nigeria.
Sobha amenukuliwa akisisitiza kuwa CAF inapaswa kuheshimu katiba na taratibu zake za kiutawala ili kuhakikisha maamuzi yote yanafanyika kwa uwazi na uhalali.
Wakati huo huo, NFF pamoja na Tume ya Michezo ya Nigeria wameeleza kuwa bado hawajapokea taarifa rasmi kutoka FIFA kuhusu hatima ya malalamiko yao, wakitoa wito kwa umma kupuuza taarifa zisizo rasmi zinazosambazwa mtandaoni.
Iwapo FIFA itaamua kuipatia Nigeria ushindi wa mezani au kuadhibu DR Congo, hatua hiyo inaweza kufungua mlango kwa Super Eagles kushiriki mechi za mchujo wa mabara kuelekea Kombe la Dunia 2026, jambo litakalofufua matumaini ya taifa hilo kurejea katika mashindano makubwa zaidi ya soka duniani.
Sakata hilo linaendelea kufuatiliwa kwa karibu barani Afrika huku wadau wakisubiri uamuzi wa mwisho wa FIFA ambao unaweza kubadilisha ramani ya uwakilishi wa Afrika katika fainali za Kombe la Dunia.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KLABU ya Simba SC imemtakia kila la heri mshambuliaji wake, Kibu Denis Prosper, baada ya kukamilisha uhamisho wake kwenda klabu ya Al Nasr SC ya Libya kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu wenye thamani ya dola za Kimarekani 250,000.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Simba usiku huu, Kibu anaondoka Msimbazi baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa misimu minne na nusu tangu alipojiunga mwaka 2021 akitokea Geita Gold.
“Baada ya kuwa sehemu ya kikosi chetu kwa misimu minne na nusu, Kibu Denis ‘Mkandaji’ ameuzwa na sasa anakwenda kuanza maisha mapya nje ya Simba SC,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Katika kipindi chake akiwa Simba, Kibu amekuwa mshambuliaji tegemeo akichangia mabao na pasi za mabao katika mashindano ya ndani na kimataifa, huku akisaidia timu kutwaa mataji mbalimbali ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho.
Uhamisho wake kwenda Al Nasr unamkutanisha tena na mshambuliaji wa Kimataifa wa Uganda, Steven Dese Mukwala, ambaye tayari alishasajiliwa na klabu hiyo ya Libya mapema.
Hatua hiyo inaonekana kuwa sehemu ya mabadiliko ya kikosi cha Simba kuelekea nusu ya pili ya msimu, huku mashabiki wakimtakia mafanikio mema Kibu katika changamoto yake mpya nje ya Tanzania.

Akizungumza kuhusu mpango huo, Mkuu wa Kitengo cha Uendelezaji Michezo wa BMT, Bw. Benson Chacha, alisema ziara hiyo inalenga pia kuhakikisha kuwa Kamati za Michezo za Mikoa zinatimiza wajibu wao wa kusimamia na kuendeleza sekta ya michezo katika ngazi za mikoa.
Kwa mujibu wa Bw. Chacha, Kamati za Michezo za Mikoa hujumuisha Afisa Tawala wa Mkoa husika, Afisa Michezo wa Mkoa, Wajumbe saba walioteuliwa na Mkuu wa Mkoa, pamoja na mjumbe mmoja kutoka kila chama au shirikisho la michezo lililosajiliwa katika mkoa husika. Aidha, Maafisa Tawala wa Wilaya na Maafisa Michezo wa wilaya zote za mkoa husika ni wajumbe wa kamati hizo.
Alisema kamati hizo ndizo zenye jukumu la kutekeleza majukumu ya Baraza la Michezo la Taifa katika ngazi ya mikoa, ikiwamo usajili wa vyama na vilabu, usimamizi wa shughuli za michezo, uendelezaji wa vipaji, uimarishaji wa miundombinu ya michezo, pamoja na kuratibu mashindano mbalimbali.
Bw. Chacha alitaja mikoa itakayotembelewa kuwa ni Kagera, Shinyanga, Simiyu, Mara, Mwanza, Geita, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Singida na Tabora.
Aliongeza kuwa tathimini hiyo inalenga pia kupima utayari wa kamati hizo katika kuendeleza sekta ya michezo, ili kuchangia kuongeza ajira, kuimarisha amani na mshikamano wa jamii, kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika michezo, na kufikia matarajio ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
“Tunataka kuona ni kwa namna gani Kamati za Michezo za Mikoa zimejipanga kuendesha michezo kwa kuzingatia misingi ya kitaifa, sambamba na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kupitia michezo,” alisema Bw. Chacha.
Aidha, alisema tathimini hiyo itaangalia hatua zilizochukuliwa na kamati hizo katika kuimarisha utawala bora, uwazi na uwajibikaji, hususan katika kusimamia shughuli za vyama na mashirikisho ya michezo ili viendeshwe kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizopo.
Bw. Chacha alisisitiza kuwa BMT itaendelea kushirikiana kwa karibu na wadau wa michezo katika ngazi zote ili kuhakikisha sekta ya michezo nchini inaendelea kukua kwa tija na kuchangia maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Mchezo huo ulisitishwa kwa takribani dakika 17 baada ya wachezaji wa Senegal kuondoka uwanjani, kabla ya mshambuliaji nyota Sadio Mané kuwashawishi kurejea na mchezo kuendelea hadi dakika za nyongeza. Senegal hatimaye walitwaa ubingwa baada ya Pape Gueye kufunga bao la ushindi katika dakika ya nne ya muda wa nyongeza, na kuipa taifa hilo taji lake la pili la AFCON ndani ya kipindi cha miaka mitano.Kwa upande wa wachezaji, CAF imewafungia washambuliaji wa Senegal Iliman Ndiaye na Ismaila Sarr mechi mbili kila mmoja kwa tabia isiyofaa dhidi ya mwamuzi. Aidha, Shirikisho la Soka la Senegal (FSF) limetozwa jumla ya faini ya Dola 615,000 ikijumuisha adhabu kwa utovu wa nidhamu wa mashabiki, wachezaji na benchi la ufundi.
Morocco nayo haikuachwa salama, ambapo beki nyota Achraf Hakimi amefungiwa mechi mbili za mashindano ya CAF, huku mshambuliaji Ismael Saibari akifungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya Dola 100,000. Shirikisho la Soka la Morocco (FRMF) pia limetozwa faini ya Dola 200,000 kwa mwenendo usiofaa wa wachezaji wake uwanjani, pamoja na Dola 100,000 nyingine kwa wafanyakazi wa kiufundi na wachezaji waliovamia eneo la VAR na kuzuia kazi ya mwamuzi.
CAF pia ilitupilia mbali ombi la FRMF la kutaka matokeo ya fainali hiyo yafutwe au kubadilishwa, ikieleza kuwa hatua za kinidhamu zilitosha na matokeo ya mchezo yanasalia kuwa halali.
Licha ya adhabu hizo, CAF imethibitisha kuwa vifungo vyote vinahusu mashindano yake pekee, hivyo havitaathiri maandalizi ya Senegal wala Morocco kuelekea Kombe la Dunia 2026 litakalofanyika Marekani, Canada na Mexico.
Katika ujumbe alioutoa kupitia mtandao wa Instagram, Kocha Thiaw aliwashukuru mashabiki kwa sapoti yao, lakini akawaomba kutoandaa michango ya kumsaidia kulipa faini hiyo, akisisitiza fedha hizo zielekezwe kwenye misaada ya dharura kwa wahitaji zaidi.




























