
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Véron Mosengo-Omba, ametangaza kujiuzulu wadhifa wake baada ya zaidi ya miaka 30 ya utumishi katika soka la kimataifa.
Katika taarifa rasmi iliyotolewa jijini Cairo Machi 29, 2026, Mosengo-Omba amesema amefikia uamuzi huo ili kujikita katika miradi binafsi baada ya kujitolea kwa muda mrefu kukuza soka kama chombo cha kuunganisha watu, kutoa elimu na kuleta matumaini.
Amesema kuwa sasa anaondoka akiwa na amani ya moyo baada ya kuondoa tuhuma zilizokuwa zikimkabili, akibainisha kuwa anaiacha CAF ikiwa imara zaidi na yenye mafanikio makubwa kuliko ilivyokuwa awali.
Mosengo-Omba pia alimshukuru Rais wa CAF, Patrice Motsepe, pamoja na timu yake na wadau wote wa soka barani Afrika kwa ushirikiano wao uliochangia mafanikio ya maendeleo ya mchezo huo.
Amehitimisha kwa kueleza matumaini yake kuwa mafanikio yaliyopatikana ndani ya CAF yataendelea kudumu na kuimarika zaidi katika siku zijazo.


Toa Maoni Yako:
0 comments: