Articles by "Haba"
Showing posts with label Haba. Show all posts

 Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Philip Besiimire (kushoto) akimkabidhi jezi ya Vodacom gwiji wa Soka Barani Afrika kutoka Nigeria, Nwankwo Kanu mbele ya wanahabari ambapo mwanasoka huyo mstaafu amekuja nchini kuunga mkono ziara ya mbio za Baiskeli za Twende Butiama 2024. Kanu, kupitia taasisi yake ya Kanu Heart Foundation, ameungana na Vodacom Tanzania Foundation kuchangia utoaji wa huduma za afya nchini kupitia ziara ya Twende Butiama 2024 katika tukio lililofanyika Makao Makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 13 Septemba, 2024.

Dar es Salaam: Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation imemkaribisha nchini Tanzania, gwiji wa Soka Barani Afrika kutoka nchini Nigeria, Nwankwo Kanu, katika ziara ya mbio za Twende Butiama mwaka 2024. Kupitia taasisi yake ya Kanu Heart Foundation, Kanu ameelezea kufurahishwa kwake kuungana na juhudi zinazofanywa na Twende Butiama kama sehemu ya kumuenzi Baba wa Taifa wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

“Ni fursa ya kipee sana kuwe sehemu ya kuleta mabadiriko kwa jamii hasa katika eneo la afya ambalo linanigusa sana. Upekee huu umenifanya nije Tanzania kuwa mmoja wa washiriki katika ziara hii kwa sababu ni jambo jema,” alisema Kanu katika mkutano na wanahabari uliofanyika Makao Makuu ya Vodacom Tanzania jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 13 Septemba, 2024.
Mbio za Twende Butiama zilianzishwa mwaka 2019 na kikundi cha waendesha baiskeli, ili kuadhimisha upendo wa Mwalimu Nyerere wa kuendesha baiskeli na maono yake kimaendeleo katika maeneo matatu muhimu ambayo ni elimu, afya, na utunzaji wa mazingira ambayo yanaweza kuwasaidia Watanzania kupiga hatua kijamii na kiuchumi.

Mkurugenzi wa Mahusiano na Vodacom Tanzania Foundation, Zuweina Farah alisema, “Tumefurahi sana Nwankwo Kanu kujumuika nasi katika mbio zetu za Twende Butiama mwaka huu, kwa kushirikiana na taasisi yake ya Moyo tunaamini itatusaidia katika msafara wetu ambapo tunatoa huduma za afya kwa magonjwa yasioambukizwa katika maeoneo kadha ya mikoa 12 tutakayopita.”
Naye mwanzilishi wa mbio za baiskeli za Twende Butiama, Gabriel Landa amesema mbio hizo zitaambatana na utoaji wa huduma kwa jamii zaidi ya afya kama vile kuchangia elimu, na kuhamasisha upandaji miti, na wanatoa nafasi kwa washiriki zaidi kujiandikisha ili kushiriki kampeni hiyo.
Dar es Salaam. Tarehe 31 Januari 2024: Katika jitihada zake za kuhamasisha matumizi ya mifumo ya kidijitali nchini, Benki ya CRDB imezindua msimu wa tatu wa kampeni ya ‘Benki ni SimBanking’ na kutenga jumla ya zawadi zenye thamani ya Shilingi milioni 470 mamilioni kwa wateja wake mwaka huu.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Wateja wadogo na wakati wa Benki ya CRDB, Bonaventure Paul amesema lengo la kampeni hiyo ni kujenga utamaduni wa matumizi ya kidijitali katika huduma za kifedha ili kuendana na kasi ya maendeleo na kuondokana na matumizi ya fedha taslimu.
“Maendeleo ya sayansi na teknolojia yanaihamisha dunia kutoka kwenye miamala ya fedha taslimu kwenda ile isiyohusisha fedha taslimu yaani cashless economy. Tanzania hatupaswi kuachwa nyuma, ni lazima twende na mabadiliko hayo tena kwa kasi inayostahili,” amesema Bonaventure.

Kushiriki na kujiwekea nafasi ya ushindi katika kampeni hiyo mteja anatakiwa kutumia SimBanking kufanya miamala yake yote ya kibenki ikiwamo kulipia ankara za maji, umeme au visimbusi vya television, ada, malipo ya manunuzi, kutuma pesa, kulipia kodi, mikopo ya kidijitali, kutoa fedha kwa ATM au CRDB Wakala, kulipia bima ya vyombo vya moto, na huduma nyenginezo.
“Kwa kadri mteja atakavyokuwa akifanya miamala mingi zaidi ndivyo atakavyojiwekea nafasi ya ushindi,” amesema Bonaventure huku akibainisha kuwa katika kampeni hiyo itakayoenda hadi mwisho wa mwaka, kutakuwa na washindi wa gari aina ya Toyota Dualis watakaopatikana kila baada ya miezi mitatu, huku zawadi za bajaj na pikipiki zikitolewa kwa mshindi wa kwanza na wa pili kila mwezi.

Aidha, katika msimu huu wa tatu wa kampeni ya ‘Benki ya SimBanking’, Benki ya CRDB imetenga zawadi za kompyuta mpakato kufikia 10 kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu, zawadi za simu janja, pamoja na fedha taslimu.

Pamoja na zawadi hizi Benki hiyo pia imetenga kiasi cha Shilingi milioni 200 zitakazotolewa kupitia Tembo Points ambazo mteja atakuwa akikusanya kila anapofanya muamala. Wateja wataweza kubadili Tembo Points zao kuwa fedha na kuzitumia kulipia huduma au bidhaa.
Bonaventure amewakumbusha wateja wa Benki ya CRDB ambao hawajakamilisha usajili wa huduma za SimBanking kukamilisha mchakato huo ili wakidhi vigezo vya kujishindia moja kati ya zawadi zilizotangazwa na kuwakaribisha wananchi wengine kufungua akaunti kwa vigezo nafuu sana na kuunganishwa na SimBanking ili kufurahia huduma zilizoboreshwa zaidi.

Benki imeendelea kuiboresha huduma yake ya SimBanking ili kutoa huduma zenye viwango vya kimataifa na uzoefu ulio bora zaidi kwa wateja. Mwaka jana, tulizindua SimBanking App iliyoboreshwa ambayo inatumia akili mnemba (Artificial intelligence), ianyoiwezesha kuwa na uwezo mkubwa katika utambuzi wa tabia na mahitaji ya mteja pindi anapotumia.

Mapema mwaka huu Benki ya CRDB imeongeza huduma mbili mpya ndani ya SimBanking ikiwamo huduma ya malipo kupitia Msimbomilia wa Taifa (TANQR) ikimuwezesha mteja kufanya malipo kwa watoa huduma wote wa Benki ya CRDB na hata mitandao ya simu. Huduma nyengine ni ile ya kujitengenezea Tembo Virtual Card mahsusi kufanikisha miamala ya kieletroniki popote pale duniani kwa kushirikiana na Union Pay.







Wanafunzi wa shule ya sekondari Uhamiaji iliyopo Kurasini jijini Dar es Salaam wakiwa katika somo la utambuzi wa vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Mkuu wa Polisi, Kitengo cha Dawati la Jinsia kata ya Kawe, ASP Elizabeth Msabira, akitoa zawadi kwa wanafunzi waliojibu vizuri wakati wa mafunzo ya elimu ya kupinga vitendo vya ukatili katika shule ya msingi Tumaini.

Wakufunzi wa mafunzo hayo wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wilayani Temeke katika shule ya msingi Mgulani.
Wanafunzi wa shule ya Mgulani wakisikiliza elimu ya utambuzi wa ukatili wa kijinsia inayotolewa na Maofisa kutoka madawati ya jinsia ya Jeshi la Polisi.

Wanafunzi kutoka baadhi ya shule za sekondari na msingi katika mkoa wa Dar es Salaam wanaendelea kunufaika kwa kupatiwa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa Kijinsia na utambuzi wa vitendo hiyo, inayotolewa na Jeshi la Polisi, kwa udhamini wa kampuni ya Barrick, ikiwa ni maadhimisho ya siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia yanayoendelea.

Shule ambazo Maofisa kutoka madawati ya kijinsia ya Jeshi la Polisi tayari wamefikisha elimu hiyo ni shule ya msingi Tumaini Kawe, Mbezi Beach, Mgulani na Sekondari za Daniel Chongolo na Uhamiaji. Mafunzo haya yataendelea kufikia shule mbalimbali za msingi na sekondari na kwenye jamii zenye mikusanyiko ya watu wengi kwenye kipindi hiki cha maadhimisho hayo.