Mkurugenzi Biashara wa Vodacom Tanzania Bw. Nguvu Kamando (wa pili kulia) pamoja na Mrajisi wa Vyama Vya ushirika nchini Dk. Benson Ndiege (wa pili kushoto) wakisaini makubaliano ya matumizi ya kidijitali kwa vyama vya ushirikia kupitia jukwaa la M-Kulima la kampuni ya Vodacom Tanzania PLC. Tukio hilo lilishuhudiwa na Mkuu wa Idara ya Mifumo ya Kidijitali wa Vodacom Tanzania Bi. Yvone Bayona (kulia) na Naibu Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika Bw. Collins Nyakunga.
*Yakabidhi kompyuta mpakato 35 kwa Tume ya Ushirika
wa Biashara wa Vodacom Tanzania Bw. Nguvu Kamando (wa pili kulia), akikabidhi moja ya kompyuta mpakato kati ya 35 zilizokabidhiwa kwa Mrajisi wa Vyama Vya ushirika Dk. Benson Ndiege (wa pili kushoto) wakati wa utiaji saini makubalino kati yao. Hafla hiyo imefanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam baada ya taasisi hizo mbili kuingia makubaliano ya matumizi ya kidijitali kwa vyama vya ushirika kupitia jukwaa la M-kulima, makao makuu ya Vodacom Tanzania jijini Dar es salaam. Tukio hilo lilishuhudiwa na Mkuu wa Idara ya Mifumo ya Kidijitali wa Vodacom Tanzania Bi. Yvone Bayona (kulia) na Naibu Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika Bw. Collins Nyakunga.
Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania Bw. Nguvu Kamando (wa pili kulia), Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika Dk. Benson Ndiege (wa pili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mifumo ya Kidijitali wa Vodacom Tanzania Bi. Yvone Bayona (kulia), Naibu Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika Bw. Collins Nyakunga (kushoto). wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wengine baada ya kusaini makubaliano ya matumizi ya kidijitali katika vyama vya Ushirikia kupitia jukwaa la M-Kulima la Vodacom Tanzania PLC.


%20(1).jpg)


Toa Maoni Yako:
0 comments: