Na Mwandishi Wetu, Nairobi

Rais wa Kenya, William Ruto, amempongeza Jaji Mohammed Abdullahi Warsame baada ya kuapishwa rasmi kuwa jaji wa 14 wa Mahakama ya Juu ya Kenya, akieleza kuwa uzoefu wake mkubwa utasaidia kuimarisha utoaji wa haki nchini humo.

Akizungumza katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Nairobi, Rais Ruto alisema ana imani kuwa Jaji Warsame ataleta mchango chanya katika mahakama hiyo ya juu kabisa nchini Kenya kupitia weledi na uzoefu wake wa muda mrefu katika sekta ya sheria.


 “Unaungwa mkono kikamilifu na tunakuombea mafanikio unapoanza jukumu hili muhimu la kulitumikia taifa letu,” alisema Ruto wakati wa hafla ya kuapishwa kwa jaji huyo.

Katika hafla hiyo pia, Rais Ruto aliwapongeza Evans Thiga Gaturu na Jedidah Wakonyo Waruhiu baada ya kutunukiwa hadhi ya Senior Counsel, akisema wameonyesha mchango mkubwa katika kuimarisha utawala wa sheria na demokrasia ya kikatiba nchini Kenya.








Ruto alisema Serikali ya Kenya itaendelea kushirikiana na mihimili mingine ya dola kuhakikisha haki inatendeka na mfumo wa sheria unaendelea kuimarika kwa manufaa ya wananchi wote.

Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Naibu Rais wa Kenya, Kithure Kindiki pamoja na Jaji Mkuu na Rais wa Mahakama ya Juu Kenya, Martha Koome.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: