WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Kikao Kazi cha 21 cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Itifaki na Uhusiano Serikalini Mei leo 7, 2026 mkoani Njombe.

Kikao kazi hicho cha mwaka, kinawakutanisha zaidi ya Maafisa Habari 300 kutoka taasisi mbalimbali za Serikali kote nchini kwa lengo la kuwanoa na kuwajengea uwezo, kusimamia na kuzifikisha kwa ufanisi taarifa za Serikali kwa umma.

Kupitia kikaokazi hicho washiriki watapata mafunzo na kufanya mijadala mizito ikiwemo ya uandishi wa kisasa wa taarifa kwa umma, mbinu za kuandika makala zenye mvuto magazetini pamoja na kanuni muhimu za itifaki katika shughuli za kitaifa.

Aidha, watapata fursa ya kujifunza kuhusu matumizi sahihi ya picha za viongozi, utaratibu wa utajo rasmi na suala la mwonekano wa mavazi katika mikutano ya kitaifa na kimataifa

Katika hatua ya kuimarisha mawasiliano ya Serikali hadi ngazi za chini, washiriki wameendelea kuhimizwa kushirikiana kwa karibu na redio za kijamii pamoja na klabu za waandishi wa habari mikoani ili kuongeza ufanisi wa utoaji wa taarifa kwa wananchi.

Sambamba na kikao hicho, wananchi wa Mkoa wa Njombe wananufaika na huduma za kibingwa bobezi zinazotolewa na wataalamu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga na Mloganzila) pamoja na Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI).

Mbali na mafunzo hayo, washiriki pia watapata fursa ya kutembelea kiwanda cha AVO AFRICA kinachozalisha mafuta ya parachichi, kushuhudia vivutio vya asili ikiwemo maporomoko ya maji ya Mpanga Kipengele, na kushiriki zoezi la upandaji miti kulinda vyanzo vya maji katika Halmashauri ya Mji wa Njombe.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: