Na Mwandishi Wetu

Jumuiya ya Tanzania Deejays Community (TDC) imepokea rasmi cheti cha usajili kutoka Baraza la Sanaa la Taifa, hatua inayotajwa kuwa mwanzo wa ukurasa mpya wa maendeleo, umoja na utambuzi wa Ma-DJ nchini.

Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Peter More amesema kupatikana kwa usajili huo ni mafanikio makubwa kwa wadau wa tasnia ya u-DJ nchini na kutatoa nafasi ya kuimarisha mshikamano na maendeleo ya sekta hiyo.

Amesema jumuiya hiyo ina matumaini makubwa ya kuendelea kukuza tasnia ya muziki na kuimarisha nafasi ya Ma-DJ katika maendeleo ya sekta ya burudani nchini.

“Tumepewa usajili rasmi na hii ni hatua muhimu inayofungua ukurasa mpya wa umoja, maendeleo na utambuzi wa Ma-DJ nchini,” alisema Dj Peter More.

Aidha, alitoa shukrani kwa Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA, Edward Buganga pamoja na timu nzima ya baraza hilo kwa ushirikiano waliouonyesha katika kufanikisha hatua hiyo.

Dj Peter More alisema Tanzania Deejays Community imeahidi kuwa mabalozi wazuri wa tasnia hiyo kwa kulinda maadili na kuendelea kusaidia juhudi za kukuza ajira kupitia sekta ya muziki na u-DJ.

Alibainisha kuwa safari ya jumuiya hiyo sasa inaanza rasmi kuanzia ngazi ya taifa, mikoa hadi wilaya kwa lengo la kuwafikia Ma-DJ wengi zaidi nchini na kuimarisha maendeleo ya tasnia hiyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: