Furaha yatamalaki Tanga Korogwe! Katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, milioni 89 zatolewa kuwainua wanawake, vijana na wenye ulemavu.
Halmashauri ya Mji Korogwe imeungana na Wanawake wa Mkoa wa Tanga kuadhimisha kilele cha siku ya Wanawake Duniani kilichofanyika Machi 08, 2026 katika viwanja vya shule ya msingi Boma huku wenyeji wakiwa ni Halmashauri ya Mji Korogwe.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Balozi Dkt Batilda Buriani amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuwawezesha wanawake kiuchumi, kijamii na kisiasa ili waweze kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Taifa. Aidha amewataka wananchi wa Mkoa wa Tanga kuendelea kudumisha upendo, amani, umoja na mshikamano ambavyo ni tunu za Taifa la Tanzania.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Korogwe Bi. Zahara Msangi ameendelea kusisitiza dhamira yake katika kuunga mkono jitihada za serikali katika kuhakikisha wanawake wanapata fursa sawa katika nyanja zote za maendeleo.

Pia ametaja faida inayotokana na mikopo inayotolewa na Halmashauri ambapo wanawake wamekua ni wanufaika wakubwa katika mkoa huo huku akiwasisitiza kuendelea kuomba mikopo hiyo kwani Halmashauri iko mlango wazi katika kuhakikisha wanawake wanaepukana na mikopo umizi.
Katika Maadhimisho hayo Halmashauti ya Mji Korogwe imekabidhi hundi yenye kiasi cha shilingi milioni themanini na tisa kwa vikundi cha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ikiwa ni kuunga mkono Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan inayotaka kumpa tabasamu mwananchi.







Toa Maoni Yako:
0 comments: