SHIRIKA lisilo la kiserikali la BRAC Tanzania limeweka mikakati zaidi kusaidia kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapa mafunzo kwenye fani mbalimbali na kuwapatia mitaji.

Wakiadhimisha siku ya wanawake duniani BRAC yenye wanachama zaidi ya 450,000 katika Mikoa 27 Tanzania wamelenga wakufikia wanawake wote kupitia vikundi vya kuweka na kukopa.

Kupitia kauli mbiu ya Siku ya wanawake duniani mwaka 2026 ni “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi kufikia Dira 2050”, ikilenga kujenga uelewa wa kuwekeza katika maendeleo jumuishi kwa kutambua na kutekeleza haki za wanawake na wasichana kwa vitendo.

‎Amesisitiza kuwa kaulimbiu hiyo imejikita katika nguzo za Dira ya Taifa ya 2050 na inahusisha makundi yote ya kijamii.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Mtaalamu wa Elimu na Mafunzo kutoka BRAC , Sophia Nyanda amesema shirika lao lina mchango mkubwa katika jamii kwani imewawezesha wasichana waliokatisha masomo kwa sababu mbalimbali ili kuweza kufikia malengo yao.

Nyanda amesema, wana mradi wa Elimu unaojulikana kama AIM ambao umeweza kuwafikia wasichana hao na kuwapa mafunzo ya fani mbalimbali na kupatiwa vifaa na kisha kuwapatia mtaji ili waweze kuendesha miradi yao.

" sisi kama BRAC tunataka kuwafikia wanawake kwa kiwango kikubwa, tunataka kufika kila mkoa ili kuwasaidia mabinti hawa ambapo baadae wakiahapata ujuzi watajiendeleza na kuendesha maisha yao bila kuwa tegemezi," amesema Nyanda.
Mtaalamu wa Masuala ya Mikopo kutoka BRAC Tanzania Bi. Graciana Rimoy akitoa elimu kwa wanawake juu ya namna ya kuweka na kukopa ili waweze kujiendeleza kiuchumi. Hayo yamefanyika katika kuadhimisha Siku ya wanawake duniani yakiwa na kauli mbiu ya “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi kufikia Dira 2050”, ikilenga kujenga uelewa wa kuwekeza katika maendeleo jumuishi kwa kutambua na kutekeleza haki za wanawake na wasichana kwa vitendo.

Kwa upande wa Mtaalamu wa Mikopo Kutoka BRAC Graciana Rimoy amesema shirika lao limekuwa linawafikia wanawake wengi kupitia mikopo ya vikundi vya kuweka na kukopa ambao kwa sasa wanahudumia zaidi ya wanawake 450,000 nchi nzima.

Amesema, wanafanya hivyo ili kuwawezesha wanawake wajiendeleze kibiashara na kabla ya kumpa mkopo huo huwa wanampa elimu ya biashara na namna ya kuweka akiba.

" tumekuwa na utaratibu wa kutoa elimu ya mikopo kwa wanawake wote ambao tunawahudumia, na hili limesaidia sana kwani wamekuwa wanaweza kuendesha biashara zao huku wakiweka akiba," amesema Rimoy.

Ameongeza kuwa, kumekuwa na wimbi la wanawake kuingia kwenye madeni ya mara kwa mara kutokana na kukosa elimu ya mikopo na namna ya uendeshaji wa biashara, ambapo ameshauri wanawake hao kuacha kutanguliza shida binafsi pindi wanapohitaji mikopo bali wazingatie vigezo na masharti ambavyo Kampuni wanaziweka.

Aidha, ameshauri Benki kuu kuweza kuweka mfumo wa pamoja wa makampuni wanayokopesha ili pindi mteja atakapokuwa anaenda kukopa iweze kuonesha taarifa za mteja huyo.

Naye Siwema Chuma mmoja wa wanufaika amewashukuru Brac kwa mazuri wanayoyatenda kwao kwani wameweza kusoma fani ya Upishi na kupewa mtaji ambao hadi sasa amesema kufungua ofisi nyingine kupitia biashara hiyo pamoja na kuajiri watu ili waweze kumsaidia.

Brac wamekuwa na utaratibu wa kutoa elimu ya mafunzo ya fani mbalimbali kwa wasichana ambapo wakishamaliza huwapatia mtaji au vifaa na kisha kuwapa mikopo ili waendeleze biashara zao.
Mwanasaikolojia na mtoa elimu Aunty Sadaka akizungumza na wanawake waliojitokeza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake mwaka 2026 yenye kauli mbiu “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi kufikia Dira 2050”, ikilenga kujenga uelewa wa kuwekeza katika maendeleo jumuishi kwa kutambua na kutekeleza haki za wanawake na wasichana kwa vitendo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: