Na Mwandishi Wetu.

Kampuni ya kubeti ya SportPesa Tanzania imeendelea kuwapa Watanzania fursa ya kubadilisha maisha yao kupitia ushindi wa jackpot pamoja na michezo mbalimbali ya kasino na Aviator, huku zaidi ya shilingi bilioni moja zikitolewa kwa washindi wa jackpot pekee katika kipindi cha mwaka uliopita.

Miongoni mwa washindi waliopata bahati hiyo ni Hamza Athman ambaye alijishindia kiasi cha shilingi 237,897,560 kupitia mchezo wa Midweek Jackpot. Ushindi huo umeelezwa kuwa umeleta mabadiliko makubwa katika maisha yake.

Akizungumza baada ya kupokea zawadi yake rasmi, Hamza alisema ushindi huo umemfungulia ukurasa mpya wa maisha na kumpa matumaini makubwa ya baadaye. Alisema siku zote alikuwa na imani kuwa ili kushinda lazima uwe sehemu ya jukwaa la SportPesa.

Mbali na jackpot, kampuni hiyo pia imeendelea kushuhudia ushindi mkubwa kupitia michezo ya kasino na Aviator, ambapo washindi hupatikana kila siku kwa kuweka dau dogo. Katika tukio moja la hivi karibuni, mchezaji mmoja aliweka dau la shilingi 420 na kufanikiwa kujishindia kiasi cha shilingi 27,964,800.

Ushindi huo unaonyesha kuwa michezo hiyo imeendelea kutoa fursa kwa wachezaji wa viwango mbalimbali, iwe ni kupitia jackpot zenye odd ndefu, ubashiri wa michezo au michezo ya kasino yenye multiplier kubwa. Wachezaji wamekuwa wakipokea ushindi wao moja kwa moja kwenye akaunti zao bila ucheleweshaji.

Akizungumzia mafanikio hayo, Mkuu wa Masoko wa SportPesa Tanzania, Tracy Humplick, alisema kampuni hiyo inaendelea kuboresha mifumo yake ili kuhakikisha wateja wanapata uzoefu bora wa kucheza na kupata ushindi wao kwa urahisi.

Alisema kampuni inawekeza katika teknolojia, huduma kwa wateja na kuboresha masharti ya michezo ili kuhakikisha uwazi, haki na uendelevu wa huduma kwa wachezaji wote.

Aidha, SportPesa Tanzania inaendelea kufanya shughuli zake kwa kuzingatia sheria na kanuni za serikali, huku pia ikichangia katika mapato ya taifa, kukuza sekta ya michezo na kutoa ajira kwa maelfu ya Watanzania.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, hadithi za washindi kama Hamza zinaendelea kuwahamasisha Watanzania wengi kujiunga na jukwaa hilo, huku zikionesha kuwa fursa ya ushindi ipo kwa kila mchezaji anayejitosa kwa nidhamu na ujasiri. Kadri idadi ya washiriki inavyoongezeka, ndivyo mzunguko wa ushindi na fursa unavyozidi kupanuka kwa Watanzania wengi zaidi.

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: