Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Mjasiriamali Daniel Deogratus Sambo, mkazi wa Kigoma Mjini, na mwanadada Doreen Masawe wameibuka washindi wa pikipiki aina ya TVS kupitia promosheni ya “Shinda Boda” inayoendeshwa na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya PigaBet.

Akizungumza baada ya kupokea zawadi yake, Sambo alisema ushindi huo ni fursa muhimu itakayomsaidia kurahisisha shughuli zake za kila siku pamoja na kukuza biashara zake.

Alisema kuwa licha ya kucheza kwa muda mrefu bila mafanikio makubwa, hakukata tamaa na hatimaye juhudi zake zimemletea matokeo chanya.

“Nilianza kucheza muda mrefu, lakini leo nimebahatika kushinda pikipiki. Hii itanisaidia sana katika shughuli zangu za kila siku na kuongeza kipato,” alisema Sambo huku akiwahimiza vijana wengine nchini kushiriki promosheni hiyo kwa uwajibikaji kwani inaweza kuwapatia fursa kama aliyopata yeye.
Katika tukio hilo, mshindi mwingine Doreen Massawe naye alieleza kufurahishwa na ushindi wake akisema pikipiki hiyo itamsaidia katika shughuli zake za kilimo na kurahisisha usafiri wakati wa kusimamia kazi zake mashambani.

“Ninajihusisha na kilimo, hivyo pikipiki hii itanisaidia sana katika kurahisisha shughuli zangu za kila siku,” alisema.
Kwa upande wake, Afisa Masoko wa PigaBet Tanzania, Hemed Msonge, alisema kampuni hiyo imeanzisha promosheni ya “Shinda Boda” ikiwa na lengo la kuwainua Watanzania kiuchumi kupitia zawadi za pikipiki zitakazotolewa kila wiki.

Alisema kuwa katika promosheni hiyo pikipiki mbili zitatolewa kila wiki kwa kipindi cha wiki sita mfululizo, hatua inayolenga kuwapa washiriki fursa ya kujiongezea kipato kupitia shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo usafiri wa bodaboda.

Msonge aliwahimiza Watanzania wengi zaidi kushiriki katika promosheni hiyo huku akisisitiza umuhimu wa kucheza michezo ya kubahatisha kwa uwajibikaji.

Aliongeza kuwa droo za promosheni hiyo zitaendelea kufanyika kila wiki hadi mwisho wa kampeni, akibainisha kuwa kaulimbiu ya kampeni hiyo ni “Cheza, shinda boda na ubadilishe maisha yako.”
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: