Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa, Jacqueline Mzindakaya, amesema maboresho ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika Kituo cha Afya cha Laela yamefikia takribani asilimia 95, huku Hospitali ya Halmashauri ya Kalambo yakifikia asilimia 88.

Mzindakaya ameyasema hayo alipofanya ziara katika Kituo cha Afya cha Laela (Wodi ya Wazazi) kilichopo Wilaya ya Sumbawanga (DC) pamoja na Hospitali ya Halmashauri ya Kalambo, ambako alikabidhi msaada wa mashuka na blanketi kwa ajili ya kuboresha huduma kwa wanawake wanaolazwa katika wodi za uzazi.
Katika Kituo cha Afya cha Laela, alikabidhi blanketi 50 na mashuka 65 kwa ajili ya kusaidia wanawake wanaojifungua na wanaopatiwa huduma katika kituo hicho.

Aidha, katika Hospitali ya Halmashauri ya Kalambo, Mbunge huyo pia alikabidhi blanketi 50 na mashuka 65 ili kuboresha mazingira ya huduma kwa wagonjwa, hususan wanawake wanaolazwa katika wodi za uzazi.

“Katika kuelekea Siku ya Wanawake Duniani, nimeona niwashike mkono wanawake wenzangu kwa kuwapatia blanketi na mashuka katika vituo hivi vya afya ili kuboresha huduma wanazozipata,” amesema Mzindakaya.

Ameongeza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuendelea kuboresha sekta ya afya na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora katika vituo vya afya nchini.

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: