

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Makongoro Nyerere, amempongeza mwanawe Prince Nyerere pamoja na mjukuu wake Charles baada ya kutwaa tuzo ya ARC2 katika mashindano ya FIA African Rally Championship.
Kupitia ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Nyerere alisema amefarijika na kujivunia mafanikio ya vijana hao, akieleza kuwa ni Watanzania wa kwanza kushinda tuzo hiyo katika zaidi ya miaka 45 ya mashindano hayo.

Aliongeza kuwa ushindi huo ni ushahidi kuwa nidhamu, bidii na uzalendo vinaweza kuzaa matokeo makubwa, huku akisisitiza kuwa mafanikio hayo yanaipa heshima familia na taifa kwa ujumla.

Vijana hao walitunukiwa tuzo hiyo Februari 15, 2026 katika hafla ya Tanzania National Motorsports Awards, hatua inayochukuliwa kama mafanikio makubwa kwa michezo ya magari nchini.


Toa Maoni Yako:
0 comments: