Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, leo Alhamis, Februari 12, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Namibia nchini, Mheshimiwa Gabriel Pandureni Sinimbo.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam, yakilenga kuendeleza na kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya vyama hivyo viwili pamoja na mataifa yao.
Katika kikao hicho, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kisiasa na kidiplomasia, wakisisitiza umuhimu wa kudumisha urafiki wa kidugu uliodumu kwa miaka mingi kati ya CCM na Chama cha SWAPO cha Namibia.
Uhusiano kati ya Tanzania na Namibia umejengwa katika misingi ya mshikamano wa kihistoria tangu enzi za harakati za ukombozi wa Afrika, ambapo Tanzania ilikuwa mstari wa mbele kuunga mkono mapambano ya uhuru wa Namibia.




Toa Maoni Yako:
0 comments: