Na Oscar Assenga,Tanga

MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi, Dkt Batilda Burian amewaomba viongozi wa dini katika mahubiri yao wawahimize waumini kuhakikisha wanajitokeza kujiandikisha Kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ikiwemo kuboresha taarifa zao.
Dkt Batilda aliyasema hayo Leo wakati akizungumza na viongozi wa dini na ya wa vyama vwanasiasa katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambapo pamoja na mambo mengine alisema zoezi la uboreshaji wa Daftari la kura litaanza February 13 mwaka huu mpaka 19.

Alisema ni upo umuhimu Makubwa viongozi hao kutumia majukwaa yao kuhakikisha wanawaelimisha waumini juu ya umuhimu wa kujiandikisha katika zoezi hilo muhimu ili kupata haki ya kuwachagua viongozi katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
"Ndugu zangu viongozi wa dini naombeni mtumie mahubiri yenu kuhakikisha mnawahamasisha wananchi kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga kura siku zimefika kesho tutakuwa na siku ya uandikishaji daftari "Alisema
"Hivyo kupitia Tume Huru ya uchaguzi walikuja na kufanya semina na viongozi wa vyama na mafunzo kwa wataalamu na Jumuiya ngazi za Kaya na Mawakala na kesho tunakwenda kwenye zoezi la uandikishaji wale vijana waliofika miaka 17 ambapo ikifika mwezi Octoba watafikisha miaka 18 wanapaswa kujitokeza kujiandikisha"Alisema

Mkuu huyo wa Mkoa alisema zoezi hilo litakwenda sambamba na la pili la kuboresha taarifa na kusahihisha taarifa ambalo pia lina umuhimu hivyo wananchi wahakikishe wanachangamkia fursa za uwepo wa zoezi hilo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: