Jamii imeaswa kuwa makini dhidi ya matapeli wa mtandaoni.
Ushauri huo umetolewa na Mtaalam wa Uchunguzi wa Udanganyifu wa Kiforensiki, Rona Katuma kutoka mtandao wa Vodacom wakati akitoa 'mada njia za kuepuka matapeli wa mitandani' mapema Makao Makuu ya Ofisi za Vodacom jijini Dar es Salaam.
Bi. Rona amesema kuna njia nne ambazo matapeli wamekuwa wakizitumia kuwatapeli wananchi ikiwemo kuuziwa bidhaa mtandaoni bila kuwajua wahusika.
"Matapeli wanatumia njia nyingi na hapa nitazielezea chache na ya kwanza ni njia ya ujumbe mfupi sms ambapo hapa unaweza tumiwa sms mtoto kadondoka shule tuma hela apatiwe matibabu akatuma njia ya pili ukapigiwa simu ukaambiwa umalizie usajili wako na kujifanya kama watoa huduma wetu", amesema Rona.
Bi. Rona amesema kuwa ni vyema wananchi wakawa makini hata kwa watoa huduma wanaozunguka mitaani (Mawakala) kwa kuacha kutoa taarifa zao binafsi kwa watu wasiowajua ambazo zinaweza kupelekea kutapeliwa.
Nae Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Tanzania, Waziri Makang'ila aliongezea kuwa (Online Scammer) zimekuwa nyingi kupitia vifaa vyetu ikiwemo Simu, Kompyuta ... tuma hela ya usajili na hapo unakuwa umetapeliwa. Amesema kuwa njia nyingine inayowaangusha vijana wengi ni ulimbukeni wa mapenzi, "Vijana wengi wamekuwa wakitapeliwa mitandaoni katika suala la mapenzi wakijiingiza kwenye mahusiano na watu wasiyowajua mitandaoni wanatapeliwa pesa mwisho wa siku wanaishia kulia", amesema.
Aliongeza kuwa ni vyema wananchi kujitokeza kukemea na kuripoti matukio ya kitapeli wa mitandaoni huku wakielekeza nguvu katika kutoa elimu ili izidi kuisambaza hasa vijijini ambapo wananchi wamekuwa na uelewa mdogo katika matumizi ya mitandao ya jamii.
Kwa upande wake Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi Tanzania, Beatrice Charles amewaomba wananchi kuendelea kujitokeza kurepoti matukio ya utapeli ili waweze kusaidiwa.
Aliwaomba wananchi kuacha kushiriki mawasiliano na watu wasiowajua maana wanakuwa wanajihatarisha na kujiweka karibu katika adha ya kutapeliwa
Mwisho Meneja huduma kwa Wateja kutoka Vodacom, Shamte Mikumuo amesema kuwa kwa sasa idadi ya wananchi wanaotapeliwa kwa njia ya kutuma pesa imepungua na kusababisha kwa siku kupokea simu za malalamiko zipatazo 20-30 tofauti na awali, ambapo hayo yote yametokana na elimu kuwa wanayopewa wananchi kuhusu masuala ya fedha katika mitandao.
"Napenda kuwaomba wananchi watambue namba rasmi ya huduma kwa wateja ni 100 ambayo unaweza kupiga au kupigiwa na si vinginevyo ukiona umezidiwa kabisa nenda katika duka letu lililokaribu nawe na tunamaduka zaidi ya 400 nchi nzima, ukishindwa tumia 0754100100 (WhatsApp)," amesema Mikumuo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: