Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini, Bw. Cosmas Saadat (kushoto) akimkabidhi msaada wa Madawati, Meza na Viti kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Babati mjini Bw Shabaani Mpendu (kulia) kwa shule ya msingi Shikizi ya Muungano Dagailoy ya Wiyala ya Babati, Manyara ikiwa ni mkakati wa kuchangia maendeleo ya elimu nchini kupitia mkakati wake wa KETI JIFUNZE unaoendelea nchi nzima. Wengine wanaoshuhudia nyuma ni Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Mhe. Getrude Gekuli, Meneja wa Tawi la CCDB Babati, Bi. Gloria Sam na Meneja mahusiano ya Kiserikali CRDB Kanda ya Kaskazini, Bw. Gabriel Kiliani.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini, Bw. Cosmas Saadat (kulia) akimkabidhi msaada wa Madawati, Meza na Viti kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Bi Anna Mbogo (kushoto) kwa shule ya sekondari ya Sarame iliyopo Babati, Manyara ikiwa ni mkakati wa kuchangia maendeleo ya elimu nchini kupitia mkakati wake wa KETI JIFUNZE unaoendelea nchi nzima.
Na Mwandishi Wetu.
Benki ya CRDB imetoa madawati 80 kwa shule ya msingi Shikizi ya Muungano Dagailoy na Meza na viti 50 sekondari ya Sarame ikiwa ni mkakati wa kuchangia maendeleo ya elimu nchini .
Akikabidhi madawati ,meza na viti hivyo meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini, Bw. Cosmas Saadat kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Babati mjini Bw Shabaani Mpendu na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Bi Anna Mbogo amesema Benki ya Crdb kupitia mkakati wake wa KETI JIFUNZE itaendelea kutoa ushirikiano kwa serikali kwa kuchangia huduma mbalimbali za kijamii Mkoani Manyara.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Bi. Anna Mbogo ameishukuru Benki ya CRDB kwa kuweza kuchangia maendeleo katika wilaya hiyo huku akizidi kuomba wadau mbalimbali kuendelea kujitokeza zaidi.
Halfa hiyo ya makabidhiano ilifanyika tarehe 19/11 /2024 ikihudhuriwa Mbunge wa jimbo la Babati Mjini Mh Getrude Gekuli, Afisa elimu msingi Babati mjini Bw. Simon Mumbee, Viongozi mbalimbali wa chama na serikali, Meneja mahusiano ya Kiserikali CRDB Kanda ya Kaskazini, Bw. Gabriel Kiliani na Meneja wa Tawi la CRDB Babati, Bi. Gloria Sam.
Wazazi na Wanafunzi wa shule ya msingi Shikizi ya Muungano Dagailoy ya Wiyala ya Babati, Manyara wakifuatilia.
Toa Maoni Yako:
0 comments: