Mkuu wa Kanda ya Kati wa Vodacom Tanzania Plc, Joseph Sayi (Kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 20 kwa mshindi wa mwezi wa kampeni ya Ni Balaa! Amina Gwila mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha Tawi la Dodoma mwishoni mwa wiki katika hafla iliyofanyika duka la Vodacom jijini Dodoma. Amina amepata nafasi ya kuchagua shule ambayo Vodacom watasaidia kukarabati maktaba yake ili kukamilisha adhma ya kusaidiana na Serikali katika kuboresha elimu nchini.
Afisa wa M-Pesa kutoka Vodacom Tanzania Plc, Mkoa wa Dodoma, Musa Kushoka (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi 500,000/- kwa mshindi wa droo ya sita ya kampeni ya Ni Balaa! Kila mtu ni mshindi, Bw. Felician Mgimba (Kulia) katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Endelea kufanya miamala na kununua vifurushi ili uweze kuibuka mshindi.
Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania Plc Mkoa wa Dodoma, Balikulije Mchome (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi 500,000/- mshindi wa droo ya sita wa kampeni ya Ni Balaa! Kila mtu ni mshindi, Bw. Peter Sheka katika duka la Vodacom lililopo jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Endelea kufanya miamala kupitia M-pesa nawe uwe mshindi.
Afisa Mauzo wa Vodacom Tanzania Plc mkoa wa Dodoma, Athumani Ngoma (kushoto) akimkabidhi mshindi wa wiki ya sita wa kampeni ya Ni Balaa! Kila mtu ni mshindi, Angel Bahingali (Kulia) mfano wa hundi ya shilingi 500,000/- katika duka la Vodacom lililopo jijini Dodoma mwishoni mwa mwiki. Endelea kufanya miamala na kununua vifurushi kupitia M-pesa ili uweze kuibuka mshindi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: