Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo akizungumza katika kongamano la uwekezaji kwenye sekta ya Utalii Jijini Arusha Leo 30 April 2024Mkurugenzi Mtendaji kituo cha uwekezaji Tanzania TIC Bw. Gilead Teri akizungumza na katika kongamano la uwekezaji katika Ukumbi wa mkutano Gran Melia Jijini Arusha, Aprili 30, 2024.
Waziri wa Maliasili na Utalii Angela Kairuki akizungumza kwenye kongamano la sekta ya Utalii katika mkoa wa Arusha 30 April 2024
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda akiwakaribisha wageni waliokuja kwenye kongamano la uwekezaji kwenye sekta ya Utalii mkoa wa Arusha leo 30April, 2024. 
Washiriki wa kongamano la uwekezaji wa Utalii lililofanyila leo 30april 2024 Katika hotel ya Garan Melia Jijini Arusha
Washiriki wa kongamano la uwekezaji wa Utalii lililofanyila leo 30april 2024 Katika hotel ya Garan Melia Jijini Arusha

Na Vero Ignatus, Arusha.

Kituo cha uwekezaji (TIC) kinatarajiwa kujengwa mkoani Arusha ikiwa ni kuondoa urasimu wanaokutana nao wawekezaji ili kupata hati na nyaraka zote kwa wakati katika kituo cha pamoja kwa lengo la kuinua uchumi.

Hayo yamesemwa leo Jijini Arusha na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo wakati akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji kwenye Sekta ya Utalii lililohudhuriwa na zaidi ya wadau 420 kutoka Serikalini, wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Prof. Mkumbo ameeleza kuwa kupitia utekelezaji wa sera na sheria mbalimbali za uwekezaji na maelekezo mahususi ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Serikali imeendelea kupata mafanikio mbalimbali katika kuhamasisha, kuvutia na kuwezesha uwekezaji nchini.

Prof. Mkumbo ameainisha mambo 10 ya msingi katika utalii ikiwemo Amani, Utulivu na Salama, Malazi miundombinu ya usafiri, Mikakati mizuri ya kutangaza Utalii, Suala la tabia njema na ukarimu wa wenyeji, uwepo wa miundombinu ya malazi, Elimu kwa watoaji huduma kwa watalii, uwepo wa mitaji kwaajili ya uwekezaji , uwepo wa idadi ya watu wenye uwezo wa kuongea lugha zaidi ya moja, kuwepo na vituo vya kujifunza lugha. na Uhusiano bora wa kimataifa

Akizungumza katika kongamano hilo Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angela Kairuki (Mb) amesema kutoka na Royal tour wameweza kufikia watalii mil 1.8 na wanajianda zaidi kuona namna ya kuongeza watalii na maeneo ya malazi ikiwemo kuandaa malazi ya madaraja mbalimbali yenye ubora, usafi pamoja na huduma zinazopatikana.

"Fursa bado zipo katika mnyororo wa thamani ambapo kwa umoja wetu utatusaidia kuboresha uchumi zaidi na kuongeza Pato Ila Lengo likiwa ni kuvuka matarajio watalii wanapokuja wapate kumbukumbu nzuri sambaba na wenyeji wasiwe ndugu watazamaji badala yake na wawe wa moja katika kuongezea pato la Taifa".

"Tunatakiwa kuongeza Utalii wa mikutano kwa kuhakikisha ukumbi huo wa AICC unakamilika kwa haraka Uwe na Tija ili wageni waweze kuvutiwa zaidi pamoja na kuliongezea Taifa kipato", Alisema.

Akieleza Maudhui ya mkutano huu Dkt. Tausi M Kida katibu mkuu ofisi ya Rais mipango na uwekezaji amesema kongamano hilo ni takwa kutoka ktk ofisi hiyo ambayo Mh. Rais aliitoa wakati akiwaapisha viongozi

Aidha amesema kuwa Utalii wa ndani unaongezeka kwa kasi hadi kufikia 1.9 mil tofauti na hapo awali, kwani mwaka 2022 Tanzania ilikuwa inapokea watalii 1.5 milioni ukilinganishwa na make 2023 watalii wameongezeka hadi kufikia million 2 amesema kwa sasa Tanzani inapokea wageni mil 4 huku changamoto ya vidanda ikiwepo132, 676

Dkt. Kida ameweza kuainisha Malengo ya kongamano hilo Kufahamu Fursa za biashara zilizopo ikiwa ni pamoja
Kufahamu mwenendo wa Fursa za Utalii na mwenendo wa Utalii nchini
Fursa za ushirikiano kupitia ofisi ya msajili wa hazina, Fursa ya kutbua na kubaini mikakati kuboresha huduma za Utalii nchini sambaba na kuongeza vitanda kwaajili ya wageni wanaoingia nchini

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda ni ombi letu kwamba Arusha kuwepo na one stop Centre kwamba mgeni anapofika aweze kuondoka na certificate yake, vile vile mkoa huu unaochangia Pato la Taifa kwa kuingiza fedha za kigeni hivyo tutahakikisha Arusha inakiwa na umeme wa kutosha

"Tunataka kamera ziwepo kila eneo la mji wa Arusha, ifikapo mwezi Julai mwaka huu Taa na watu wanafanya shughuli zao ni la kubughudhiwa, Barabara zetu mkoa wa Arusha ni mbovu na ni aibu kubwa labda nimuulize Dada yangu Angela Kama wameamua barabara hizi ziwe kivutio cha watalii sawa Sisi hatuna tatizo tutarendelea kupromote la sivyo tupeni pesa kwaajili ya kutengeneza barabara "Tumekubaliana na Tanrod tunakwenda kuondoka mabango yote Arusha na tunaweka eletronic"

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekezaji (TIC) Bw. Gilead Teri amesema kuwa katika uwekezaji wa kukuza na kuimarisha Sekta ya Utalii nchini, Serikali ya awamu ya sita imeweka mikakati mbalimbali ili kuhakikisha, wananchi wanafanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta hiyo, ikiwa ni pamoja na kutoa msamaha wa ushuru na punguzo la kodi kwa wawekezaji.

Teri amesema kuwa, kutokana na ongezeko la idadi ya watalii inayotokana na programu ya Tanzania Royal Tour iliyofanywa na Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan mwaka 2022, imeandaa Sera inayolinda mtaji wa Mwekezaji kwa kushusha kodi kutoa dola 1,000 mpaka kufikia laki 5 na dola elfu 50 kwa wazawa huku ikitoa msamaha wa ushuru mpaka pale mtaji utakapoanza kutoa faida.

"Tunataka mtaji wa Mwekezaji utumike kukuza mtaji wake badala ya kulipa mrundikano wa kodi, na kuruhusu kuanza kulipa kodi mara baada ya kutengeneza faida, hali ambayo licha ya kutoa unafuu kwa wawekezaji inasaidia kuvutia wawekezaji wengi zaidi wazawa na wageni kuwekeza kwenye sekta ya Utalii" Amesema Terry

Aidha, ameyataja malengo ya Kongamano hilo ni pamoja na kuwajulisha wadau fursa zinazopatikana kwenye sekta ya utalii na nafuu mbalimbali zilizowekwa na Serikali kupitia sheria ya Uwekezaji ya mwaka 2022 na kusisitiza wawekezaji kuwa huu ni mwaka wa kutengeneza faida kupitia sekta hiyo.

Amefafanua kuwa, Kongamano hilo litatoa fursa ya kuwasilisha fursa, zinazopatikana kwenye sekta ya utalii, mawasilisho yatakayochochea majadiliano kati ya watalamu na wadau waliopo kwenye sekta ya Utalii mkoani Arusha, ili kujua fursa na changamoto zilizopo ili kuongeza kiwango cha uwekezaji kwenye sekta hiyo.

Aidha Kongamano hilo limeanyika kufuatia maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyoyatoa wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali mwanzoni mwa mwezi Aprili, 2024, akimtaka Mkuu wa Mkoa wa Arusha, kushughulikia changamoto ya upatikanaji wa vyumba vya kulala wageni wanaotembelea Mkoa wa Arusha

Kongamano hilo limebeba "Kauli Mbiu ya Uwekezaji Katika Utalii Endelevu, Uchangamkiaji wa fursa za Uwekezaji baada ya Program ya Tanzania 'The Royal Tour'.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: