Timu ya Uhusiano kwa umma kutoka Kampuni ya Blanq Marketing and Communication Agency ikiongonzwa na Mkurugenzi wake, Asinati Eliafie (kushoto) wamekuwa ni miongoni mwa maelfu ya wakimbiaji walioshiriki mbio za Kili Marathon mkoani Kilimanjaro hapo Jana.

Akizungumza baada ya kutimua mbio hizo za nyika, Asinati Eliafie amesema wamefanya hivyo ili kuwaunga mkono wateja wao ambao pia wamedhamini mbio hizo na wengine wakiwa tu washiriki wa kawaida.

Anaongeza kuwa anafurahi kuona kazi za wateja wao ambazo zinafanywa na Kampuni yao ya Blanq Marketing and Communication zinawafikia maelfu ya Watanzania.

Mbio hizo zenye hadhi ya kimataifa, zimefanyika Jana kwa kuanza na kumalizika katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika, Moshi mkoni Kilimanjaro.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: