Mkuu wa Mkoa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga, leo Januari 20, 2024 amefungua kikao cha 5 cha Baraza la Kwanza la Wafanyakazi la Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).Kikao hicho kinalenga kujadili mapendekezo ya Bajeti ya fedha mwaka 2024/2025.
Akiwa Katika ufunguzi huo RC Sendiga, amesisitiza umuhimu wa kikao hicho mabacho kinasaidia kujenga na kushauri uongozi katika mambo mbalilimbali ya kiutumishi na upangaji bajeti.
Mkurugeni Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ameeleza kuwa Mkoa wa manyara utanufaika na mpango wa Mawasiliano ambapo Mkoa umepata Minara 32 ambayo ipo katika hatua za wali za utekelezaji pamoja na kuongeza nguvu minara 12 ambapo mpaka sasa imeshaongezwa nguvu minara 6.
Aidha, Mhe Sendiga ameipongeza Taasisi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) pamoja na Chama cha wafanyakazi TUGHE kwa kazi kubwa wanayoifanya kwani ni kiuongo muhimu kati ya Watumishi na serekali.
Toa Maoni Yako:
0 comments: