Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga amekuwa mgeni rasmi katika kikao kazi na wadau wa mbegu za mazao kilichoandaliwa na Tume ya ushindani (FCC) Kanda ya Kaskazini.

Kikao kazi hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuwahusisha wadau mbalimbali wakiwemo wakulima, wauzaji wa mbegu za mazao, maafisa ugani kilikuwa na lengo la kujadili hali ya ushindani wa kibiashara katika upatikanaji, uzalishaji na usambazaji wa mbegu za mazao nchini.

Mhe. Sendiga amesema kuwa ili biashara iweze kuwa na tija ni lazima ifanywe kwa kufuata taratibu, miongozo kanuni na sheria zilizowekwa. 
Aidha amewatahadharisha wafanyabiashara juu ya vitendo viovu vinavyo fifisha ushindani katika biashara kama vile kupanga bei moja, kupanga na kuzalisha aina moja ya bidhaa n.k.

“Ni lazima kila mwenye biashara awe na kitu chake, awe na bei zake lakini kwa kufuata sheria, kanuni, miongozo na taratibu ili kuleta ushindani” akisisitiza Mhe. Sendiga.

Mwisho amesema serikali awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan imekuwa kinara katika kuinua sekta ya kilimo na wakulima kupitia uanzishwaji wa viwanda vidogo na vikubwa vya uzalishaji na kuweka mazingira ya amani kwa wafanyabiashara.
Wadau mbalimbali wakiwemo wakulima, wauzaji wa mbegu za mazao, maafisa ugani wakifuatilia katika kikao kikichoandaliwa na FCC kwa lengo la kujadili hali ya ushindani wa kibiashara katika upatikanaji, uzalishaji na usambazaji wa mbegu za mazao nchini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: