Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, Halima Okash (kushoto) na Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Maajar Trust, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar wakikata utepe wakati wa uzinduzi wa jengo la darasa la Kompyuta lilojengwa kwa msada na Taasisi hiyo katika Shule ya msingi Majengo Bagamoyo Pwani Taasisi hiyo ilipata msaada wa Kompyuta hizo kutoka taasisi ya Nos Vies en Paratage Foundation (NVEP) inayofadiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow. Watatu kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Hassan Maajar Trust, Sharif Maajar, wengine ni walimu wa shule hiyo.Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, Halima Okash (kulia) Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Maajar Trust, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar na Makamu mwenyekiti wa taasisi hiyo Bw. Sharif Maajar, wakiangalia mwanafunzi wa shule hiyo Jasimi Juma wakati akijifunza kutumia kompyuta mara baada ya uzinduzi wa jengo la darasa la Kompyuta lilojengwa kwa msada na taasisi hiyo katika Shule ya msingi Majengo Bagamoyo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Maajar Trust, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar akiongea wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Pwani, Halima Okash (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Maajar Trust (HMT), Balozi Mwanaidi Sinare Maajar, cheti maalumu cha kutambua mchango wa HMT wakati wa hafla hiyo,kushoto ni Makamu Mwenyekiti Bw.Sharif Maajar.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Pwani, Halima Okash akiongea katika hafla hiyo
Wanafunzi wa shule ya msingi Majengo wakifanya onyesho la muziki wa zilipendwa wakati wa hafla hiyo.
Na Mwandishi Wetu.
Taasisi ya Hassan Maajar Trust (“HMT”), imeendeleza dhamira yake ya kuboresha mazingira ya shule za msingi nchini, ambapo leo imekabidhi darasa la kompyuta pamoja na kompyuta kumi na tatu (13) kwa shule ya msingi Majengo iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani.
Jengo hilo lililogharimu jumla ya Shillingi milioni Thelathini na Mbili 32,000.00 na Dola 10,000.00 kwa ajili ya kompyuta kumi na tatu zilizofadhiliwa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVep) inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow. Gharama za ujenzi ni kubwa kidogo kwa kuwa shule haina uzio hivyo ikabidi kuweka madirisha imara ili kulinda kompyuta zitakazokuwa darasani.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Maajar, Balozi Mwanaidi Maajar, alikabidhi darasa na kompyuta hizo kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bi. Magdalena Tiothem Amsi katika hafla fupi iliyofanyika mwishoni mwa wiki na iliyohudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mheshimiwa Bi Halima Okash, ambaye alikuwa mgeni rasmi, wawakilishi wa Barrick, Maofisa kutoka Kitengo cha elimu , walimu na wanafunzi.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Halima Okash, ambaye alikuwa ndiye mgeni rasmi, aliipongeza, HMT, kwa kuamua kuzikabili changamoto za kuboresha mazingira ya elimu kwa kutoa misaada ya madawati, huduma za maktaba, kujenga miundombinu ya vyoo na sasa darasa la kompyuta pamoja na kompyuta kwa shule ya Msingi Majengo. “Kwa niaba ya serikali nawapongeza kwa jitihada mnazofanya kuboresha mazingira ya kupata elimu mashuleni” alisema.
Akiongea katika hafla hiyo, Balozi Maajar alisema “Hii ni sehemu ya utaratibu wa taasisi ya HMT kuasili shule na kubaki hapo kufanya ujenzi au ukarabati wa majengo na miundo mbinu ya kusomea hadi ikiwa imetangamaa ndiyo wanaondoa uasili”. Kwa sasa wanaendelea kuomba wabia kushirikiana kufanya ukarabati mkubwa wa madarasa 5 hapo shuleni Majengo.
Aidha alisema kuwa “kwa kipindi kirefu nyuma, HMT ilikuwa inajulikana kwa kampeni yake kubwa ya ‘Dawati Kwa Kila Mtoto’ ambayo imefanikiwa kwa kutoa madawati 10,000, na kunufaisha Zaidi ya wanafunzi 30,000 katika mikoa 13 nchini. Tuliona vilevile kuna haja ya kufundisha elimu ya kompyuta shule zetu za msingi kwa sababu ni jambo lisilokwepeka katika muktadha wa dunia ya leo.
Aidha alisema, kila safari ni hatua ya kwanza na kwa mradi huu ndiyo hatua ya kwanza kwa HMT kutimiza lengo la kuiborehsa shule hii iliyoiasili ili ipate kuwa mfano wa kuigwa kwa wafadhili na watu wenye nia njema kuunga juhudi za Serikali katika kuboresha elimu nchini”.
Alisema Kupitia hafla tofauti za ukusanyaji fedha kama vile ‘Fundraising Gala’ na ‘Matembezi ya Hiyari’, HMT kupitia kampeni ya Dawati kwa Kila Mtoto ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuhamasisha umma kuona kuwa wajibu wa kuboresha mazingira ya shule zetu si wa Serikali pekee na kuweza kuchangia madawati mengi lakini changamoto hii bado ipo kutokana na ongezeko la wanafunzi baada ya seara ya Serikali ya elimu bure kwa kola mtoto. Kwa HMT ni faraja kubwa kuona idadi kubwa ya watoto wetu siku hizi wakiwa hawakai tena chini.
Mwakilishi wa Barrick katika hafla hiyo, Georgia Mutagahywa, alisema kuwa NVep na Barrick imeona fahari kushirikiana na HMT katika mradi huu kwa kuzingatia umuhimu wa suala la TEHA katika shughuli nyingi za kazi na maendeleo ya mtu binafsi na nchi kw aujumla. Barrick inatambua umuhimu wa Watoto kuanza kujifunza masuala ya TEHAMA mapema na imefurahi kupata fursa ya kuchangia katika jambo hili muhimu.
Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi ya Majengo, Bi. Magdalena Tiothem Amsi, aliishukuru taasisi ya HMT kwa kutoa msaada huo ambao alisema “utawezesha wanafunzi wa shule hiyo kusomea katika mazingira rafiki na hasa kwa hili darasa wanfunzi wa Majengo wataweza kuwa na elimu ya TEHAM ambayo kwa sasa ni muhimu sana duniani kote”, alisema.
Taasisi ya Hassan Maajar inafanya maandalizi ya kukarabati madarasa 5 hapo shuleni Majengo na wanaomba wafadhili na wabia wao kusaidia kuchangia kutimiza lengo hilo.
HMT ina imani watu wengi wataendelea kuhamasika kushiriki kwa kutambua kuwa ni jukukumu letu sote kuborehsa mazingira ya kusomea kwa watoto wetu ambao ndiyo taifa la kesho na siyo tu kazi ya serikali peke yake.
Toa Maoni Yako:
0 comments: