Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia, Mheshimiwa Nape Nnauye akizungumza na wageni waalikwa kwenye ukumbi wa Mlimani city kupitia teknolojia ya hologramu, iliyomwezesha kuonekana kama yupe ukumbuni hapo kiuhalisia lakini hakuwepo hapo. Hii ni baada ya Vodacom kuzindua rasmi mtandao wa 5G. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Hilda Bujiku
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Hilda Bujiku
Baadhi ya wadau wa teknolojia wakijadili mapinduzi ya kidigitali yanayotarajiwa kuletwa Tanzania na 5G
---
Dar es Salaam. Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC imezindua huduma ya mpya teknolojia 5G ikisema italeta mapinduzi na kuongeza ushiriki wa Taifa katika kuleta mageuzi ya nne ya viwanda.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Septemba Mosi, 2022 na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Hilda Bujiku wakati wa halfa ya uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City.

"Teknolojia hii ya 5G inakuja na fursa kubwa hapa nchini kwa wabunifu kuleta bidhaa na huduma mpya kwa wananchi. Vodacom sio tu itaendelea kubuni huduma mpya bali kuwezesha jamii ili kutimiza ndoto za kujenga Taifa bora.

Katika uzinduzi huo, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye aliyeeleza kuwa, Mei mwaka huu aliahidi Bungeni kwamba Tanzania itaanzisha 5G hapa nchini jambo hilo limetia leo kwa kampuni ya Vodacom kulitekeleza.

"Tuliposema ilikuwa kama ndoto lakini leo karibu miezi mitatu, lakini Vodacom wametekeleza na kutusaidia kuingia kwenye orodha ya nchi chache Afrika zilizoanzisha huduma ya teknolojia ya 5G.Vodacom wamekuwa wa kwanza kwenye mambo mengi wameanza na M-Pesa na mambo mengine nawashukuru," amesema Nape.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: