Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt Dorothy Gwajima akifafanua Jambo jijini Dar,kuhusu kuelekea Siku ya Familia Duniani,ambapo nchini kilele cha siku hiyo kimepangwa kuwa ni Mei 15,2022.
Na WMJJWM, Dar Es Salaam
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt. Dorothy Gwajima ikiwa zimesalia siku chache kufikia Kilele cha Siku ya Familia Duniani hapo Mei 15, 2022, ameendelea kutoa Elimu kwa Jamii juu ya umuhimu wa Malezi Bora ndani ya Familia.
Akiwa Jijini Dar es Salaam, Mei 10 2022, Mhe. Gwajima amevifikia Vituo vya Azama Media, Clouds Media na TBC Taifa kwa lengo la kufafanua mambo mbali mbali kuelekea Siku ya Kimataifa ya Familia.
Akiwa katika Vituo hivyo kwa nyakati tofauti, Dkt. Gwajima amesema, kuundwa kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum na yeye kupewa dhamana na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni dhamira njema aliyo nayo Mhe. Rais katika kusukuma ajenda ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii ikiwepo mambo ya Familia.
"Kama unavyofahamu, Wizara hii haina muda mrefu ina takribani ni miezi mitatu tangu kuundwa kwake lengo la uwepo wa Wizara hii ni kusukuma ajenda ya Maendeleo kwa wananchi na mambo kama haya ya siku ya Familia na Maadhimisho mengine" alisema Dk. Gwajima.
Dkt. Gwajima akiongea, wakati Wizara hiyo alisema Wizara hiyo wakati ikiwa pamoja na Afya mambo mengi yalikuwa hayapewi msukumo Mkubwa kutokana na kwamba hata Wizara ya Afya nayo ilikuwa na mambo mengi hivyo maono ya Mhe. Rais katika kuundwa kwa hii Wizara ni ishara kwamba mambo mengi yaende na yatokee.
Dkt. Gwajima alisema kwa Mwaka 2022, Siku ya Familia itafanyika kimkoa kwa kila Mkoa kuadhimisha kwenye Mkoa wao huku wakiongozwa na waheshimiwa Wakuu wa Mikoa na kwa Ngazi ya Wizara wao wataungana na Mkoa wa Dodoma lakini akasema pia Mgemi Rasmi anatazamia kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
Siku ya Familia kwa Mwaka 2022 inaongozwa na kaulimbiu “Dumisha Amani na Upendo kwa Familia Imara; Tujitokeze Kuhesabiwa.” Kauli mbiu hii inaleta Dhahiri Amani na Upendo katika Familia vinavyowezesha familia kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya watoto kiafya, kielimu kimaadili na katika shughuli za kiuchumi. Familia yenye uchumi imara itaweza kumudu kutoa huduma bora za lishe, elimu na ulinzi dhidi ya vitendo vya ukatili.
Toa Maoni Yako:
0 comments: